TANGAZO

TANGAZO
WEKA TANGAZO LAKO HAPA

Alhamisi, 26 Septemba 2013

Waislamu kote duniani waimarishe umoja'



'Waislamu kote duniani waimarishe umoja'
Rais Hassan Rohani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa maulamaa na shakhsia wa Kiislamu nchini Marekani ni nembo ya umoja na mshikamano wa Waislamu.
Rais Rohani aliyasema hayo jana alipokutana na maulamaa, wasomi na walinganiaji wa Kiislamu katika jamii ya Marekani na kusisitiza kuwa ulimwengu wa Kiislamu hii leo unahitajia umoja na mshikamano zaidi kuliko wakati wowote mwingine. Ameongeza kuwa maulamaa na shakhsia wa Kiislamu wa Marekani wanaweza kutoa mchango muhimu katika kukurubisha pamoja mataifa mawili ya Iran na Marekani na kutatua migogoro ya Mashariki ya Kati.
Rais Rohani amesema kuwa walinganiaji wa Kiislamu wanawajibika kutumia mbinu bora zaidi za kueneza dini na kusema kuwa, inasikitisha kwamba hii leo propaganda za kuwatisha watu kuhusu Uislamu zinafanywa kwa kiwango kikubwa.
Amesema kuwa Ulimwengu wa Kiislamu na eneo la Mashariki ya Kati linasumbuliwa na matatizo mengo baada ya uingiliaji wa nchi za kigeni, misimamo ya kufurutu mipaka, ukatili na ugaidi na akaongeza kuwa la kusikitisha zaidi ni kwamba baadhi ya ukatili huo unafanyika kwa kutumia jina la dini. 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni