Jamani waislamu tusipelekwe tu kama magari mabovu na hawa bakwata kwasababu sijui niwaweke katika kundi gani yaani hawana hata aibu wanatangaza edd jumatano haliya kua watu wana simama arafa kesho waislamu tuamke tuacheni kulala jamani.
hii ndo taarifa yao hebu isome. chanzo bakwata.

Baraza kuu la waislamu Tanzania (Bakwata) limetangaza
rasmi kwamba sikukuu ya Eid adh'ha maarufu kama Eid el hajj itakuwa siku ya jumatano tarehe 16 oktoba mwaka huu.
Katika taarifa yake iliyotoa kwa vyombo vya habari imesema kitaifa swala ya Eid el Hajj itafanyika katika msikiti wa Al Farouk ulioko makao makuu ya baraza hilo Kinondoni jiji dar es salaam.
Sikukuu ya Eid el hajj hufanyika kila mwaka baada ya waislamu walioko Makka kumaliza ibada yao tukufu ya kufanya Hijja.
Aidha, imesuniwa kufunga kwa waislamu masiku kumi ya mwezi wa dhulhijja na yule ambaye atashindwa kufanya hivyo basi ajitahidi afunge ndani ya mwezi Tisa ya Dhulhijja.
Kumekuwa na mabishano ya kihoja kwa waislamu kuhusu ipi siku sahihi ya kufunga mwezi tisa ya Dhulhijja, kama ni ile ya mahujaji wanaposimama katika viwanja vya Arafa au mwezi Tisa kulingana na mwandamo wa mwezi wa sehemu mtu aliyokuwepo.
Kumeelezwa kwamba funga ya mwezi tisa ilikuwepo kabla ya kufaradhishwa ibada ya Hijja.
UAE (united Arab Emirates, دولة الإمارات العربية المتحدة) mwezi Agosti 25, mwaka huu ilitangaza sikukuu ya Eid el Hajj itakuwa tarehe 15 oktoba.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni