TANGAZO

TANGAZO
WEKA TANGAZO LAKO HAPA

Alhamisi, 26 Septemba 2013

Askari wa kulinda amani wa UN wabaka nchini Mali



Askari wa kulinda amani wa UN wabaka nchini Mali
Ripoti zinasema kuwa askari wasiopungua wanne wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wameshiriki katika ubakaji nchiniMali.
Askari hao ni miongoni mwa wanajeshi 1,500 wa Chad wanaohudumu katika Opereshini ya Kurejesha Amani ya Umoja wa Mataifa nchini Mali (MINUSMA).Tukio hilo limeripotiwa kutokea Septemba 19 ambapo wanajeshi hao walimbaka mwanamke mmoja katika mji wa kaskazini mwa Mali wa Gao. Umoja wa Mataifa umeitaka Chad kuchunguza suala hilo na kuwaadhibu wahusika.
Askari 6,000 wa Kiafrika walipelekwa kuhudumu katika kikosi cha kulinda amani nchini Mali, baada ya Ufaransa kuishambulia nchi hiyo Januari 11 mwaka huu kwa kisingizio cha kupambana na waasi wa kaskazini mwa Mali.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni