Kundi la Boko Haram limeua watu wasiopungua 27 katika mashambulizi mawili tofauti yaliyofanyika huko kaskazini mwa Nigeria.
Afisa wa serikali ya Nigeria Alhaji Modu Gana Sheriff amewaambia waandishi habari kuwa watu 27 wameuawa na wapiganaji wa kundi la Boko Haram katika mashambulizi mawili tofauti yaliyofanyika kwenye mji wa Gamboru katika jimbo la Borno.
Serikali ya Nigeria imekata mawasiliano ya simu katika jimbo la Borno katika jitihada za kujaribu kuvuruga mashambulizi ya Boko Haram na kwa sababu hiyo inachukua muda habari muhimu kutangazwa.
Vurugu na machafuko yamezidi katika majimbo ya kaskazini mwa Nigeria tangu Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria aliamuru jeshi la nchi hiyo kukomesha uasi wa kundi la Boko Haram mwezi Mei mwaka huu
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni