Waziri Mkuu wa Ethiopia amekosoa hali ya machafuko na ukiukwaji wa haki za binadamu unaoshuhudiwa katika nchi nyingi za Afrika hususan katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Haile Mariam Desalegn ameliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba nchi za Afrika zinaendelea kusumbuliwa na machafuko na ukiukwaji wa haki za binadamu na kwamba hali hiyo inatia wasiwasi mkubwa.
Waziri Mkuu wa Ethiopia pia ametuma salamu za rambirambi kwa taifa, serikali na familia za wahanga waliouawa katika shambulizi la kigaidi kwenye jumba la madula la Westgate nchini Kenya na kusisitiza kuwa, tukio hilo linaonesha tena udharura wa jamii ya kimataifa kupambana na ugaidi na misimamo ya kufurutu mipaka. Amesema machafuko yanayotokea katika nchi za Afrika hususan katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yanatishia usalama na amani na kwamba njia pekee ya utatuzi ni kuzikutanisha pande hasimu katika meza ya mazungumzo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni