Akizungumza pambizoni mwa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Walid al Muallim ameongeza kuwa, kwa wananchi wa Syria Bashar ni Rais aliyechaguliwa kuongoza nchi hadi katikati ya mwaka ujao wa 2014, ambapo uchaguzi mwingine wa rais utafanyika. Ameongeza kuwa, serikali ya Damascus itawakaribisha wagombea wengine kushiriki uchaguzi huo kwa mujibu wa katiba na kwamba taifa la Syria ndilo lililo na haki ya kuchagua kiongozi wake.
Aidha Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria amesema, magaidi wanaopigana nchini humo wanaungwa mkono na nchi jirani kama Uturuki na Jordan pamoja na baadhi ya nchi za Kiarabu kama vile Saudi Arabia na Qatar.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni