TANGAZO

TANGAZO
WEKA TANGAZO LAKO HAPA

Jumamosi, 28 Septemba 2013

maalim seif afunguka kuhusu muungano

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Seif Sharrif Hamad amesema mgogoro wa Muungano uliopo unatokana na kufichwa kwa makubaliano yaliyowekwa na waasisi wa Muungano  na hivyo kusema kuwa kero hizo hazitokwisha hadi kuwepo kwa Serikali tatu na Muungano wa mkataba.

Aliyasema hayo juzi wakati wa kongamano la Wanzanzibar waishio Bara na kusema kuwa Muungano uliotiwa saini na waasisi wa Muungano huo umefichwa na hivyo kutaka dawa yake ni kuwepo kwa Serikali tatu na  Muungano wa mkataba.

Seif Sharif Hamad ambaye pia ni Makamo wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, alimtaka Rais Jakaya Kikwete kutosaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba 2013 kwa maelezo kuwa una kasoro.

“Wanzanzibar wenzangu mimi pia ni mmoja wa Wanzanzibar ambao tunataka Muungano wa mkataba---nilipoulizwa na tume nilisema nataka Muungano wa mkataba—nadhani nanyi pia mawazo yenu ni kama mimi” alisema Hamad

Hamad aliisifu Serikali ya Kikwete kwa kuwaachia wananchi  wenyewe kuiandika Katiba yao  na hivyo kumtahadharisha kutokuwa na wazo la kutia saini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba 2013.

Alisema Zanzibar ni nchi kamili yenye mamlaka kama ilivyo kwa nchi nyengine hivyo inahitaji kurejeshewa mamlaka yake na kuwa na maamuzi ikiwa na pamoja kurejeshewa kiti chake katika Baraza la Umoja wa Kimataifa.

“Zanzibar iko na haki ya kuingia mikataba na jumuiya za kimataifa kama ilivyo nchi nyengine---tunataka dola ya Zanzibar iliyo nchi kamili kama ilivyokuwa zamani---Muungano umeifuta Zanzibar katika ramani ya kimataifa” alisema na kuongeza

“Hivi sasa Zanzibar haina haki ya kusema inajiunga na jumuiya yoyote ya kimataifa---kikwazo hiki ni kufichika kwa makubaliano ya Muungano kutoka kwa waasisi wetu ambao tunasema umefichwa” alisema Seif Sharif Hamad

Alisema ili kuondoa migogoro na manung’uniko za pande zote mbili ni kuwepo kwa Serikali tatu na Muungano wa mkataba jambo ambalo litaondosha kelele zote za Muungano na kupelekea ustawi wa jamii na  umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi.

Kiongozi huyo aliwataka Wanzanzibar wanaoishi Bara kwa pamoja kushikamana na kutunza umoja wao na kuhakikisha Katiba Mpya inaweka madai yao likiwemo la kutaka Muungano wa mkataba.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni