Wakimbizi wengine wazama baharini
Wakimbizi kadhaa wanahofiwa kuwa wamekufa baada ya mashua yao kuzama karibu na kisiwa cha Sicily, katika bahari ya Mediterenia nchini Italia.
Watu 250 wanasemekana kuwa walikuwamo katika mashua hiyo iliyozama umbali wa maili 70, kutoka pwani ya kisiwa cha Italia cha Lampedusa.
Shirika la Habari nchini Italia Ansa limesema takribani miili 50, ikiwa ni pamoja na wanawake na karibu watoto 10, imeondolewa baharini.
Waziri Mkuu wa Italia Enrico Letta amesema kiasi ya manusura 150 wameokolewa na meli nyingine ya Malta.
Wiki iliyopita wakimbizi zaidi ya mia tatu walikufa maji karibu na kisiwa hicho cha Lampedusa.
Mashua hiyo iliyokuwa inawasafirisha wakimbizi mita tano ilizama baada ya kuwaka moto.
Idadi kubwa ya wakimbizi walikuwa wanatoka Eritrea na Somalia.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni