TANGAZO

TANGAZO
WEKA TANGAZO LAKO HAPA

Alhamisi, 26 Septemba 2013

KENYA YAANZA KUCHUNGUZA SHAMBULIO LA WESTGATE



Kenya yaanza kuchunguza shambulio la Westgate


Mashirika ya kijasusi ya Marekani, Uingereza na Israel yanaisaidia Kenya kuchukunguza shambulio lililofanywa katika jengo la maduka la Westgate jijini Nairobi na kupelekea watu wasiopungua 72 kuuawa na kuharibiwa sehemu ya jengo hilo.

Afisa mwandamizi wa Kitengo cha Kitaifa cha Operesheni za Majanga amesema kuwa, uchunguzi huo ni kwa ajili ya kupata taarifa ambazo zitasaidia kufahamu utambulisho wa magaidi na uraia wao kikiwemo kipimo cha DNA.

Hayo yanajiri huku kundi la al Shabab lililotangaza kuhusika na shambulio la Nairobi likisema kwamba, shambulio la Westgate ni tahadhari kwa nchi za Magharibi na Kenya na kwamba, wanapaswa kuondoa askari wao nchini Somalia la sivyo watakabiliwa na umwagaji damu zaidi. Kwa mujibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya, zaidi ya watu 67 wameuawa wakiwemo maafisa sita wa Jeshi la Ulinzi la Kenya huku wengine karibu 200 wakijeruhiwa.
 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni