BIN HAFIDH
ASALAM ALAYKUM WAJA WA ALLAH
TANGAZO
WEKA TANGAZO LAKO HAPA
Alhamisi, 26 Septemba 2013
Rais Kikwete ana kwa ana na Melinda Gates
Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete,akifanya mazungumzo na Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi ya Melinda � Gates Foundation,Melinda Gates huko New York Marekani
Rais wa
Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete, amekutana na kufanya mazungumzo na Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi ya Melinda – Gates Foundation, Melinda Gates.
Rais Kikwete na Melinda Gates walikutana juzi kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, ambako wote wawili wamehudhuria mikutano ya kimataifa inayoendelea kwenye makao makuu hayo.
Katika mazungumzo hayo, Rais Kikwete na Melinda Gates walizungumzia miradi mbali mbali ambayo taasisi hiyo inaunga mkono na kugharimia Tanzania katika maeneo ya afya ya jinsi ya kupunguza na kumaliza vifo vya akinamama na vifo vya watoto wadogo pamoja na shughuli za kilimo.
Katika mazungumzo hayo, Melinda Gates alimpongeza Rais Kikwete kwa uongozi wake katika maeneo hayo na pia ameipongeza Tanzania kwa mafanikio makubwa katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDG’s) hasa katika maeneo ya elimu na chanjo kwa watoto.
“Mheshimiwa Rais, nyie katika Tanzania mmepata mafanikio ya ajabu kabisa katika suala la elimu na katika utoaji wa chanjo kwa watoto wadogo kupambana na magonjwa mawili makubwa yanayoua watoto wadogo, yaani magonjwa ya kuharisha na homa ya mapafu,” alisema Melinda
Gates.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni
Chapisho Jipya
Taarifa za zamani
Nyumbani
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni ( Atom )
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni