Rais Kikwete alitoa kauli hiyo juzi jioni baada ya kutembelea kituo cha utafiti cha Taasisi ya Afya Ifakara (IHI) kilichoko katika Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kuangalia utendaji kazi wake.
Alisema kama mgonjwa wa mwisho wa malaria nchini Marekani alionekana mwaka 1956, basi angependa mgonjwa wa mwisho wa malaria nchini Tanzania aishie mwaka 2016.
Aliipongeza IHI kwa juhudi zake za kufanya utafiti mbalimbali za dawa na chanjo.
Aidha, Rais Kikwete, alipata fursa ya kutembelea kituo hicho cha IHI Bagamoyo na kujionea changamoto mbalimbali zinazokikabili pamoja na kupata maelezo ya utendaji kazi wake.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa IHI, Dk. Salim Abdallah, alimweleza Rais Kikwete, shughuli za kituo hicho pamoja na changamoto mbalimbali zinazokikabili.
Dk. Abdallah alisema umuhimu wa kuwapo kwa IHI- Bagamoyo hapa nchini ni pamoja na kuwezesha kufanyika kwa tafiti tiba za awali ikiwa ni hatua ya kwanza kuelekea uwezekano wa kutengeneza chanjo za magonjwa ya binadamu na uwezo wa kutathmini dawa na chanjo katika hatua za mwanzo katika tafiti tiba.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni