TANGAZO

TANGAZO
WEKA TANGAZO LAKO HAPA

Ijumaa, 4 Oktoba 2013

Mazungumzo ya kitaifa Tunisia kuanza kesho

Tunisia

Duru ya kwanza ya mazungumzo ya moja kwa moja kati ya chama tawala cha an Nahdha nchini Tunisia na vile vya upinzani yenye lengo la kutatua mivutano ya kisiasa, itaanza hapo kesho nchini humo
. Muungano wenye ushawishi mkubwa wa wafanyakazi wa UGTT ambao umechukua jukumu la kupatanisha mgogoro wa kisiasa ulioanza kutokota mwezi Julai mwaka huu nchini Tunisia umetangaza kuwa, kikao hicho kitawashirikisha viongozi wa ngazi za juu wa vyama vyote vya siasa nchini humo. Taarifa ya muungano huo imeeleza kuwa, hatua hiyo imefikiwa baada ya kufanyika mazungumzo ya kina kati ya Hussein Abbas mkuu wa muungano huo na Rashid al Ghanoushi mkuu wa chama cha an Nahdha. Mgogoro wa kisiasa nchini Tunisia ulishtadi mara baada ya kuuawa Muhammad al Brahimi mmoja wa viongozi mashuhuri wa upinzani nchini humo. Imeelezwa kuwa, Masalafi wenye misimamo mikali ndio waliotekeleza shambulio hilo la kigaidi dhidi ya al Brahimi. Amma wapinzani wanakinyooshea kidole cha tuhuma chama cha an Nahdha kuwa ndicho kilichohusika na mauaji ya al Brahimi na Shokri Belaid kiongozi wa muungano wa upinzani wa Popular Front nchini humo

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni