TANGAZO

TANGAZO
WEKA TANGAZO LAKO HAPA

Jumatatu, 30 Septemba 2013

Chuo kilichovamiwa Nigeria kilikosa ulinzi


Maafisa wa utawala nchini Nigeria wanasema kuwa hapakuwa na ulinzi katika chuo cha mafunzo ya kilimo nchini Nigeria ambako hadi wanafunzi 50 waliuawa Jumapili.

Wabunge, Kenya - wakimbizi waondolewe



Kamati ya bunge inayohusika na ulinzi na uhusiano na mataifa ya kigeni imependekeza kufungwa kwa kambi za wakimbizi nchini Kenya, ikisema zinatishia usalama wa nchi.

Jumapili, 29 Septemba 2013

MTOTO ALIYEFARIKI NA KUZIKWA MIAKA MIWILI ILIYOPITA AONWA NA MAMA YAKE AKIWA HAI‏..MATUKIO KATIKA PICHA

Mtoto Shabani Maulidi akiwa tayari melala kitandani katika hospitali ya wilaya ya Geita.

Boko Haram yaua watu 27 Nigeria



Kundi la Boko Haram limeua watu wasiopungua 27 katika mashambulizi mawili tofauti yaliyofanyika huko kaskazini mwa Nigeria.

‘Hatari ya silaha za nyuklia za Israel izingatiwe’


‘Hatari ya silaha za nyuklia za Israel izingatiwe’


Msemaji wa Jumuiya ya Kiislamu ya Colombia amesema kuwa, walimwengu wanapaswa kuzingatia hatari ya silaha za atomiki za utawala wa Kizayuni wa Israel. Rashid Caravali amesisitiza kwamba, umewadia wakati sasa kwa nchi za Mashariki ya Kati na nchi nyingine ulimwenguni kuipa uzito hatari ya silaha za nyuklia za utawala haramu wa Israel hasa kwa kuzingatia kwamba, utawala huo mara kadhaa wa kadhaa umeonesha wazi na bila kificho uadui wake kwa nchi za eneo. Msemaji wa Jumuiya ya Kiislamu ya Colombia ameongeza kuwa, Israel sio tu kwamba, inamiliki silaha za kemikali bali inazo pia silaha za nyuklia ambazo ni tishio kubwa kwa usalama wa dunia hususan eneo la Mashariki ya Kati. Rashid Caravali amesema, jamii ya kimataifa inapaswa kuushinikiza utawala huo ghasibu ili uangamize silaha zake zote za atomiki na kwa muktadha huo eneo la Mashariki ya Kati litashuhudia amani na utulivu.

Al-Mualim: Mpango amani umshirikishe Assad

Al-Mualim: Mpango amani umshirikishe Assad



Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria amesema kuwa, serikali ya Damascus haitokubali mpango wowote wa amani wa kukabidhi madaraka kwa ajili ya nchi hiyo ambao hautomshirikisha Rais Bashar al Assad.

Matamshi ya Rais wa Tunisia yaighadhibisha Imarati


Matamshi ya Rais wa Tunisia yaighadhibisha Imarati


wwwbinhafidhi


Umoja wa Falme za Kiarabu, Imarati umemwita nyumbani balozi wake wa nchini Tunisia kulalamikia wito wa Rais wa nchi hiyo Moncef Marzouki kutaka Muhammad Morsi, rais wa Misri aliyeondolewa madarakani na jeshi na kuwekwa kizuizini hadi sasa, aachiliwe huru. Akihutubia mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa juzi Alkhamisi, Rais wa Tunisia aliwataka watawala wapya wa Misri wanaoungwa mkono na baadhi ya nchi za Kiarabu ikiwemo Imarati wamwachie huru Rais halali wa nchi hiyo Muhammad Morsi aliyeondolewa madarakani Julai 3 katika mapinduzi yaliyoongozwa na jeshi. Gazeti la Al- Khaleej linaloakisi misimamo ya serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu limekosoa hotuba ya Rais wa Tunisia kwa kuishambulia serikali ya mpito ya Misri na kusisitiza kuwa kinachotakiwa kufanywa ni kuiunga mkono serikali ya Cairo ambayo imekuja madarakani kwa matakwa ya wananchi. Baada ya jeshi kumuondoa madarakani Morsi, Umoja wa Falme za Kiarabu, Saudi Arabia na Kuwait ziliunga mkono mapinduzi hayo na kuahidi kuipatia kwa pamoja Misri msaada wa dola milioni 12 kusaidia uchumi wake uliozorota…/

Mashambulizi ya ash- Shabab katika kambi ya wakimbizi ya Daadab Kenya






wwwbinhafidhi.blogspot.comWimbi la mashambulio ya kundi la ash- Shabab la Somalia katika nchi jirani lingali linaendelea. Katika hatua yao ya hivi karibuni wanamgambo wa ash- Shabab wameshambulia kambi ya wakimbizi ya Daadab huko kaskazini mwa Kenya. Ripoti zinaeleza kuwa watu watatu wameuliwa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mashambulizi hayo. Imeelezwa kuwa wafanyakazi wa shirika moja la kimataifa la huduma za kibinadamu pia wamelengwa kwa mashambulizi hayo ya ash-Shabab.
Kambi ya wakimbizi ya Daadab iko katika mpaka wa Kenya na Somalia na ndio kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani. Maafisa usalama wa kieneo wameeleza kuwa wavamizi wa ash-Shabab walikuwa wamejizatiti kwa silaha za aina mbalimbali na mada za milipuko na waliingia kwa nguvu kambini hapo. Kambi hiyo inawahifadhi wakimbizi wengi wa Kisomali wasio na ulinzi waliokimbia ukame na mapigano ya ndani nchini kwao.
Jumamosi iliyopita pia watu wengi waliuliwa na wengine kujeruhiwa katika mashambulizi yaliyofanywa na kundi hilo hilo la ash-Shabab katika jengo la maduka la Westgate jijini Nairobi, Kenya.
Tangu mwaka jana wanamgambo wa kundi la ash-Shabab walianza kupoteza ngome zao muhimu nchini Somalia na kulazimika kurudi nyuma baada ya kupata kipigo kutoka kwa vikosi vya majeshi ya Umoja wa Afrika vilivyopelekwa nchini humo kusaidia serikali ya Mogadishu. 
Wakati huohuo kufukuzwa wanamgambo wa ash-Shabab katika bandari ya kistratijia ya Kismayu ambayo ilikuwa moja ya ngome zao kuu, kulikuwa na umuhimu mkubwa. Hii ni kwa sababu sehemu kubwa ya mahitaji ya silaha na chakula ya wanamgambo wa ash-Shabab ilikuwa ikidhaminiwa kupitia bandari hiyo.
Harakati za kundi hilo la ash Shabab zimezilazimisha nchi mbalimbali za Kiafrika kuchukua tahadhari kubwa za kiusalama. Huko Uganda vikosi vya usalama vimejiweka tayari kwa ajili ya kukabiliana na mashambulizi yoyote yanayoweza kufanywa na kundi hilo. Miongoni mwa hatua hizo ni kufungwa kamera kwenye maeneo ya umma, barabarani na katika baadhi ya majengo na vilevile kuimarishwa hatua za kiulinzi kwenye mipaka ya Uganda.
Uganda ni miongoni mwa nchi zilizochangia wanajeshi katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika huko Somalia. Kundi la ash-Shabab linapinga vikali uingiliaji wa vikosi vya majeshi ya kigeni huko Somalia na linataka vikosi hivyo viondoke katika ardhi ya nchi hiyo. Awali wanamgambo wa ash-Shabab walitishia kwamba watalipiza kisasi iwapo vikosi vya nchi za kigeni havitaondoka Somalia.
Mlipuko wa bomu uliotokea Kampala mji mkuu wa Uganda wakati watu walipokuwa wakitazama fainali za mpira wa miguu za Kombe la Dunia mwaka 2010 zilizofanyika Afrika Kusini na kuua  watu 76, ni mfano mmoja wa hatua za kulipiza kisasi za kundi la kigaidi la ash-Shabab huko Uganda. Wanamgambo wa ash-Shabab wamedai kuwa, wanajeshi wa Kenya wameondoka huko Somalia kutokana na hali mbaya ya usalama inayoikabili Kenya, madai ambayo yamekadhibishwa na viongozi wa Nairobi.  
Swali linaloulizwa kwa sasa ni kuwa, ni nani anayewafadhili na kuwadhaminia wanamgambo wa ash-Shabab silaha na mahitaji mengine muhimu?  Wakati huo huo weledi wa mambo wanasema kuwa ukosefu wa amani katika eneo la Pembe ya Afrika unayafaidisha madola ya Magharibi ambayo yatatumia fursa hiyo kwa ajili ya kuingilia masuala ya ndani ya nchi za eneo hilo.

Mlipuko waua watu 6 huko Tumbuktu Mali


Mlipuko waua watu 6 huko Tumbuktu Mali

Watu 6 wameuawa wakiwemo raia wawili na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia mlipuko uliotokea karibu na kambi ya jeshi katika mji wa kihistoria wa Timbuktu nchini Mali. Afisa wa serikali katika eneo hilo ameeleza kuwa, mlipuko huo wa kutegwa garini umesababisha pia nyumba kadhaa kuporomoka na kutokea hasara kubwa.
Serikali ya Mali imelaani shambulio hilo lililotokea ikiwa zimepita siku chache tu tangu waasi wa Tuareg wanaopigana ili kulitenga eneo la Kaskazini wasimamishe mazungumzo na serikali, wakiituhumu kwamba imeshindwa kuheshimu makubaliano ya amani yaliyofikiwa kati ya pande mbili. Mwezi Juni viongozi wa kundi la Tuareg walifikia makubaliano na serikali ya mpito ya Mali yaliyopelekea kurejea jeshi kwenye mji wa Kidal na kufanyika uchaguzi wa rais.

Serikali ya Kenya imesema nchi iko katika vita na wapiganaji wa Somalia, al Shabaab.


Wakenya wakiomboleza kwa kuwasha mishumaa nje ya Westgate

Imekanusha kuwa vitisho vya mashambulio vinavotolewa na kundi hilo vilipuuzwa.
Jumamosi usiku wafiwa na marafiki walioonesha majonzi waliwasha mishumaa nje ya Westgate kuwakumbuka waliokufa.Inajulikana kuwa watu 67 walikufa katika shambulio la Westgate, liloendelea kwa siku nne.
Magazeti ya Kenya yameandika ilani inayodaiwa kutolewa na idara ya usalama mwaka mmoja uliopita kuhusu watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa al-Shabaab mjini Nairobi ambao wakipanga mashambulio ya kujitolea mhanga, piya katika jengo la maduka la Westgate.
Magazeti ya Kenya yameuliza iwapo wakuu walishindwa kuchukua hatua baada ya onyo hilo na mengine yaliyofuata; pamoja na onyo moja kwamba kutafanywa mashambulio sambamba mijini Nairobi na Mombasa baina ya tarehe 13 hadi 20 Septemba.
Kamati ya bunge itayokutana Jumatatu imeonesha inataka kutazama swala hilo la ilani hizo zilizotolewa.
Afisa mmoja mwandamizi wa wizara ya mambo ya ndani alisema serikali inapata taarifa kama hizo kila siku.
Hatua zimechukuliwa kuepusha mashambulio mengi.
Alisema Kenya iko vitani, na kila siku kijana wa Kenya anashawishiwa na al-Shabaab kuuwa Wakenya.

boko haram la shambulia nigeria


Ramani ya Nigeria

wwwbinhafidhi.blogspot.comJeshi la Nigeria linasema watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Kiislamu wa kundi la Boko Haram wameshambulia wanafunzi waliolala katika chuo cha kilimo katika jimbo la Yobe, kaskazini mwa nchi.
Inaarifiwa kuwa wapiganaji waliwafyatulia risasi wanafunzi wa chuo hicho katika eneo la mashambani la Gujba.
Inaarifiwa piya kuwa walichoma moto madarasa .
Duru za hospitali kaskazini-magharibi mwa Nigeria zinasema watu kama 26 wameuwawa katika shambulio hilo.

Kenya: Maafisa walikuwa na taarifa

Vikosi vya usalama vilipambana na magaidi wa Al Shabaab waliowaua wakenya wengi wasio na hatia

Mawaziri wa serikali walipokea taarifa kuhusu tisho la mashambulizi ya kigaidi kabla ya kundi la Al Shabaab kushambulia jengo la Westgate mjini Nairobi.
Kwa mujibu wa taarifa za kijasusi zilizofichuliwa, zilionyesha maelezo ya mipango ya mashambulizi hayo kufanyika Nairobi au mjini Mombasa.
Mawaziri wanne na mkuu wa majeshi walikuwa wamefahamishwa kuhusu tisho la kufanyika shambulizi la kigaidi.
Watu 67 walifariki na mamia kujeruhiwa katika shambulizi la kigaidi ambalo Al Shabaab walikiri kulifanya Septemba 21 mjini Nairobi.
Kwa mujibu wa taarifa za gazeti la Daily Nation, mawaziri walipokezwa taarifa za kati ta yarehe 13 na 20 kuhusu uwezekano wa kufanyika mashambulizi kadhaa ya kigaidi mjini Mombasa na Nairobi.
Onyo hizo zilitolewa kwa mara ya kwanza mnamo mwezi Januari kwa mujibu wa gazeti hilo na kwa mara nyingine kuanzia Septemba.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, serikali ya Israel pia ilitoa taarifa za kuonya kuwa huenda magaidi wakashambulia majengo yanayomilikiwa na raia wake kati ya tarehe 4 na 28 Septemba.
Daily Nation limeripoti kuwa taarifa za kijasusi zilionyesha kuwa viongozi wa al-Shabab walikuwa wameanza kulenga maeneo ya kushambulia ikiwemo Westgate na kanisa la Holy Family Basilica.
Kuna hofu idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka.
Maafisa wa serikali wanaosemekana kupokea taarifa hizo ni pamoja na waziri wa fedha, Julius Rotich, waziri wa usalama Joseph Ole Lenku, waziri wa maswala ya kigeni, Amina Mohammed, waziri wa ulinzi Raychelle Omamo na mkuu wa majeshi Julius Karangi.
Mkuu wa shirika la ujasusi Michael Gichangi, anatarajiwa kuhojiwa na kamati ya bunge kuhusu usalama siku ya Jumatatu.

Jumamosi, 28 Septemba 2013

Kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka 30, viongozi wa Marekani na Iran wamezungumza moja kwa moja.



Rais Rouhani na ObamaRais Rouhani na Obama

Rais Barack Obama na mwenzake wa Iran, Hassan Rouhani, wamezungumza kwa simu kwa muda wa robo saa; na kwa mujibu wa Bwana Obama walieleza azma yao ya kutatua mzozo wa muda mrefu kuhusu mradi wa nuklia wa Iran.
Ujumbe kwenye mtandao wa Twitter kutoka ofisi ya Bwana Rouhani ulionesha hisia kama hizo.
Taarifa kutoka Iran zinaonesha kuwa tukio hilo limefurahiwa nchini humo, hasa kati ya washauri wakuu wa Bwana Rouhani.

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda anatarajiwa kufungua Kongamano la siku mbili la Uwekezaji kanda ya Kaskazini kesho



wwwbinhafidhi.blogspot.com

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda anatarajiwa kufungua Kongamano la siku mbili la   Uwekezaji kanda ya Kaskazini kesho pamoja na maonyesho ya kibiashara na Utalii ambapo wageni wa ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kuhudhuria.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa alisema Pinda anatarajiwa kuwasili kesho (leo) ambapo jumla ya wageni 450 wanatarajiwa kuhudhuria.

Alisema Kongamano hilo la siku mbili litashirikisha halmashauri 33 za kanda ya Kaskazini ambapo kila moja itajifunza na kueleza namna ambavyo halmashauri yake inavyoendeshwa.

“Waziri Mkuu Mizengo Pinda ndie atakaeongoza kongamano letu la siku mbili pamoja na kufungua maonyesho ya kibiashara—hii  ni fursa nzuri ya  wenye viwanda na biashara kujitangaza” alisema na kuongeza

“Kongamano hili litakuwa na mapinduzi kwa halmashauri zetu hasa kwa hii kanda ya kaskazini kwani baada ya hapo tunataka kufanya kazi kwa vitendo na sio kwa nadharia” alisema Gallawa

Gallawa alisema kongamano hilo ambalo lengo lake ni kuwashawishi wawekezaji kujionea fursa zilizopo za uwekezaji kanda ya kaskazini  pamoja na miundombinu mizuri ya kusafirisha bidhaa kwa kutumia barabara, reli na bandari zikiwa zinapatikana.

Alisema Mikoa ya kanda ya Kaskazini iko na fursa nyingi za uwekezaji lakini inashindwa kujitangaza na hivyo kuonelea kuitisha kongamano hilo pamoja na wawekezaji kujionea wao wenyewe.

“Mimi nadhani baada ya kongamano hili wawekezaji watajua kuwa kweli eneo letu linafaa kwa uwekezaji na ninaamini maisha ya wananchi yatabadilika na umasikini utapungua” alisema Gallawa

Alisema kongamano hilo ambalo litaenda sambamba na maonyesho ya biashara na kazi za asili zinazotengenezwa  ndani na kuwataka wananchi kujifunza kupitia kongamano hilo ambalo ni nafasi adhimu kwao na kwa Mk

maalim seif afunguka kuhusu muungano

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Seif Sharrif Hamad amesema mgogoro wa Muungano uliopo unatokana na kufichwa kwa makubaliano yaliyowekwa na waasisi wa Muungano  na hivyo kusema kuwa kero hizo hazitokwisha hadi kuwepo kwa Serikali tatu na Muungano wa mkataba.

Aliyasema hayo juzi wakati wa kongamano la Wanzanzibar waishio Bara na kusema kuwa Muungano uliotiwa saini na waasisi wa Muungano huo umefichwa na hivyo kutaka dawa yake ni kuwepo kwa Serikali tatu na  Muungano wa mkataba.

Seif Sharif Hamad ambaye pia ni Makamo wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, alimtaka Rais Jakaya Kikwete kutosaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba 2013 kwa maelezo kuwa una kasoro.

“Wanzanzibar wenzangu mimi pia ni mmoja wa Wanzanzibar ambao tunataka Muungano wa mkataba---nilipoulizwa na tume nilisema nataka Muungano wa mkataba—nadhani nanyi pia mawazo yenu ni kama mimi” alisema Hamad

Hamad aliisifu Serikali ya Kikwete kwa kuwaachia wananchi  wenyewe kuiandika Katiba yao  na hivyo kumtahadharisha kutokuwa na wazo la kutia saini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba 2013.

Alisema Zanzibar ni nchi kamili yenye mamlaka kama ilivyo kwa nchi nyengine hivyo inahitaji kurejeshewa mamlaka yake na kuwa na maamuzi ikiwa na pamoja kurejeshewa kiti chake katika Baraza la Umoja wa Kimataifa.

“Zanzibar iko na haki ya kuingia mikataba na jumuiya za kimataifa kama ilivyo nchi nyengine---tunataka dola ya Zanzibar iliyo nchi kamili kama ilivyokuwa zamani---Muungano umeifuta Zanzibar katika ramani ya kimataifa” alisema na kuongeza

“Hivi sasa Zanzibar haina haki ya kusema inajiunga na jumuiya yoyote ya kimataifa---kikwazo hiki ni kufichika kwa makubaliano ya Muungano kutoka kwa waasisi wetu ambao tunasema umefichwa” alisema Seif Sharif Hamad

Alisema ili kuondoa migogoro na manung’uniko za pande zote mbili ni kuwepo kwa Serikali tatu na Muungano wa mkataba jambo ambalo litaondosha kelele zote za Muungano na kupelekea ustawi wa jamii na  umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi.

Kiongozi huyo aliwataka Wanzanzibar wanaoishi Bara kwa pamoja kushikamana na kutunza umoja wao na kuhakikisha Katiba Mpya inaweka madai yao likiwemo la kutaka Muungano wa mkataba.

sudan nako kwanuka hakukaliki

50 wauawa kwenye ghasia Sudan

wwwbinhafidhi.blogspot.com

Ghasia zilianza Jumatatu serikali ilipoondoa ruzuku kwa mafuta
Maafisa wa usalama nchini Sudan wamewaua watu 50 katika maandamano yaliyofanywa kwa siku kadhaa kupinga hatua ya serikali kuondoa ruzuku ya mafuta. Taarifa hii ni kwa mujibu wa mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini humo.
Polisi waliwatupia gesi ya kutoa machozi waandamanaji zaidi siku ya Ijumaa.

Waandamanaji wameikosoa serikali ya Rais Omar al-Bashir kwa hatua hii na kumtaka aondoke mamlakani.Maafisa wanasema kuwa chini ya watu 29 wamefariki na kusema kuwa serikali ilikuwa haiwezi tena kumudu gharama ya ruzuku ya mafuta.
Taasisi ya elimu ya maswala ya haki na amani pamoja na shirika la Amnesty International zimesema kuwa watu wamepata majeraha ya risasi kwenye vifua na vichwa kulingana na jamaa, madaktari na waandishi wa habari.
Kijana mwenye umri wa miaka 14 alikuwa miongoni mwa waathiriwa wengi waliokuwa kati ya umri wa miaka 19-26. Waliongeza kusema kuwa mamia ya watu wamezuiliwa.
"Kuwaua kwa kuwapiga risasi watu kwenye vifua na vichwani ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na Sudan lazima isitishe ghasia hizi mara moja,’’ alisema Lucy Freeman, Naibu mkurugenzi wa shirika la Amnesty International.
Duru za hospitalini zimeambia BBC kuwa takriban watu 60 wameuawa.
Maafis wa serikali ya Sudan bado hawajasema chochote kuhusu mauaji hayo lakini waziri wa habari Ahmed Belal Osman alisema kuwa idadi ya vifo ambayo ni juu zaidi ya watu 29 sio sawa.
Ghasia zilianza Jumatatu pale serikali ilipoondoa ruzuku kwa mafuta ili kupandisha ushuru. Hatua ya serikali kupunguza gharama ya matumizi ya pesa za umma, ilisababisha kupanda kwa bei ya mafuta na kuwaathiri sana watu wa kipato cha chini.

allwa mkubwa hatuna budi ya kumshukuru

dd
dunia ina mamboooooooooooooooooo hebu vuta pichaaaaaaaa kama ndo................................












Wakuu wa usalama kuhojiwa Kenya

hili ndio jengo la westgate nchini kenya  hapa ni ya sehem moja ya jengo hilo lilovyoporomoka


Maafisa wakuu wa ujasusi wametakiwa kufika mbele ya kamati ya ulinzi ya bunge ili kuhojiwa kuhusu mashambulizi ya kigaidi dhidi ya jumba la Westgate mjini Nairobi.
Taarifa kwenye vyombo vya habari nchini humo zinaonyesha kuwa hali ya kulaumiana imeanza kuibuka huku mashirika ya usalama yakinyosheana kidole.

Wataalamu wa uchunguzi wa mauaji wangali wanafanya uchunguzi wao wakitafuta miili na dalili za kilichosababisha shambulizi hilo.Watu 67 waliuawa kwenye shambulizi hilo huku zaidi ya miamoja sabini na tano wakipata majeraha mabaya. Shirika la Red Cross nalo linasema kuwa watu 61 wangali hawajulikani waliko.
Kamati ya bunge inataka maafisa wanaohusika na maswala ya usalama waweze kuwajibishwa.
Kundi la kigaidi la nchini Somalia, al-Shabab limedai kufanya mashambulizi hayo yaliyodumu siku nne kama hatua ya kulipiza kisasi kwa Kenya kujihusisha nchini Somalia kijeshi.
Hii leo ni siku ya tatu ya maombolezi kwa wathiriwa wa shambulizi hilo wakiwemo raia na wanajeshi.
Rais Uhuru Kenyatta amehudhuria mazishi ya mpwa wake na mchumba wake mjini Nairobi ambapo aliwahutubia waumini.

Walipuuza onyo?

Hatua ya kuwataka maafisa hao wa usalama kufika mbele ya tume ya bunge siku ya Jumatatu, inakuja kutokana na wasiwasi miongoni mwa wakenya kuhusu kiwango cha maafisa hao kujiandaa kwa tukio lolote la kigaidi sawa na lililotokea Westgate.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari mmoja wa maafisa waliotakiwa kufika mbele ya kamati hiyo ni mkuu wa shirika la ujasusi Michael Gichangi, anayesema alitoa taarifa za ujasusi kuhusu shambulizi hilo kwa polisi.
Lakini, afisaa mmoja mkuu katika idara ya polisi alikana kuwa taarifa hiyo ilitolewa kwa polisi.

Ijumaa, 27 Septemba 2013

UTATA MKUBWA UMEGHUBIKA TUKIO LA UGAIDI KENYA-IDADI YA VIFO, MATEKA NA MAGAIDI NI SINTO FAHAMU


Pambano lililodumu kwa Takribani sku 4 kati ya Alshababu na Majeshi ya Ulinzi ya Kenya lilifkia Tamati Juzi baada ya Rais Kenyata ku- declare pubicly kuwa The Mall is Completely rescued.

Lakini Utata mwingi umeghubika Tukio hili,hali iliyofanya Baadhi ya wanaharakati na Vyombo vya Habari nchini Kenya kuhoji Uwazi wa zoezi zima la uwokoaji ikiwemo Idadi ya Vifo, Mateka na Magaidi pia
 

Awali Rais wakati akihutubia Taifa Mchana mishare ya saa 6 kuwa tayari Majeshi yameshinda palitokea milindino ya Risasi Mithiri ya Majibidhano kati ya Majeshi na Magaidi Mjengoni mda mfupi badae hii ilidumu kwa takribani Saa nzima na kujirudia tena saa 1jioni, hali hii ilizua waswas kuwa huenda bado Magaid yalikuwemo pa1 na kauli ya Raisi, Watu wanahisi kuwa Rais aliwahi kutangaza ushindi Mapema kabla ya Magaidi yote hayajawa Kontrolled, Na kama ni hivyo ni kwa Mantiki ipi Watu wamekuwa wakihoji.
 

Sinitojua nyingine ni kuhusu MATEKA waliokuwa ndani ya Jengo ambao serikali iltangaza wawli kuwa kulikuwa na Mateka zaidi ya 150 walokuwa wameshikiliwa mjengoni, Cha ajabu baada ya zoezi kuisha ni watu wachache sana waloweza kuonekana idadi isyofka hata 30, hakuna Mateka alionekana akitoa ushahidi wa jinsi walvyotekwa ndani na waliishije wakiwa humo kama mateka kwa hzo cku 4, hofu ilizid maradufu baada ya Al Shababu jana kutangaza wazi kupitia Mtandao wao kuwa waliua Mateka 157, Hofu imetanda zaidi na Serikali huenda ina siri nzito kuhusu hili.
 

Wakati wa zoezi la kuoa lilipofikia hatua flani waandishi wa habari woote walifukuzwa na Majeshi ya Ulinzi, Chombo flani cha habari kilichokuwa kimeweka kambi kama Mita 300 toka kwenye eneo la Tukio kilishuhudia Ambulances na Magari ya Majeshi yakija kwa jasi hadi kwenye labgo la Jengo hilo na kisga kuondoka kwa spidi kali kuelekea kusikojulikana, hali hii ilidumu siku nzima ya 3 na ya 4. Watu wanafjiri Huenda ni Miili ya Mateka walokuwa wameshikiliwa na kuuawa na Magaidi au kuuawa kufatia majibizano ya risasi kati ya Majeshi na Magaidi,Serikal haikuweka wazi hapa
 

Hofu nyingine ni kuhusu idadi ya vfo imekuwa ikitofautiana awali Red Cross walidai vifo kufkia 68 lakini badae Rais Kenyatta alltangaza watu 62 kupoteza Maisha, Wakati vyombo na Mashirika ya habari toka magharibi vnadai Watu zaidi ya 70 kupoteza Maisha.
 

Tunaifanyia Tanesco mageuzi makubwa-JK


Jakaya-Kikwete-September27-2013                                                                                  Rais Jakaya Kikwete
Rais Jakaya Kikwete, amesema serikali yake inalifanyia mageuzi muhimu na marekebisho makubwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa nia ya kuharakisha jitihada za serikali kusambaza umeme kwa wananchi wengi zaidi.
Rais Kikwete aliyasema hayo jana alipokutana na kuzungumza na ujumbe wa Shirika la Misaada ya Maendeleo la Marekani la Millennium Challenge Corporation (MCC) ukiongozwa na Mtendaji Mkuu wake, Daniel Yohannes.
Yohannes alimwelezea Rais Kikwete kuhusu maendeleo ya ombi la Tanzania kuingizwa katika awamu ya pili ya misaada ya Serikali ya Marekani kupitia MCC chini ya Akaunti ya Milenia Tanzania (MCA(T)).
Nchi nyingine za Afrika ambazo maombi yao yanafikiriwa katika awamu hiyo ya pili ni Morocco, Msumbiji na Lesotho.
Tanzania ndiyo nchi iliyopokea sehemu kubwa zaidi ya msaada wa MCC duniani katika awamu ya kwanza ambapo ilipewa dola milioni 698 za Marekani.
Fedha hizo zimeingizwa katika miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara, usambazaji wa umeme vijijini, miradi ya maji na ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mafia.
Serikali ya Tanzania imeamua kuwa fedha za awamu ya pili ya MCC, zitaingizwa kupanua zaidi huduma za umeme na ujenzi wa barabara za vijijini kwa nia ya kuongeza idadi ya Watanzania wanaopata huduma za umeme na kwa nia ya kuboresha barabara za vijijini katika maeneo yanayozalisha mazao kwa wingi zaidi.
Serikali imeliweka suala la usambazaji umeme kwa Watanzania mijini na vijijini miongoni mwa maeneo yake ya kipaumbele.
Wakati anaingia madarakani mwaka 2005, ni asilimia 10 tu ya Watanzania waliokuwa wanapata umeme.
Yohannes alitaka kujua ni hatua zipi serikali inazichukua kurekebisha changamoto zinazoikabili Tanesco na hatua zinazochukuliwa kuzidi kukabiliana na matatizo ya rushwa.
Rais Kikwete alimweleza Yohannes: “Kama unavyojua, Tanesco imepitia safari ngumu na kukabiliwa na changamoto nyingi, lakini sasa tumeamua katika serikali kulifanyia mageuzi muhimu na marekebisho makubwa kwa maana ya muundo wake na pia kuangalia viwango vya malipo ambayo shirika hilo linawatoza wateja wake. Mageuzi haya katika Tanesco ni muhimu sana na yameanza kufanyika na kwa hakika serikali imedhamiria kukayamilisha mageuzi hayo kati

warioba aipiga kijembe serikali


WARI
                                                                                      Jaji Joseph Warioba

Tume ya Mabadiliko ya Katiba imelishangaa Bunge kwa ‘undumila kuwili’ wake wa kupitisha sheria mbili zinazokinzana kuhusiana na mchakato unaosimamiwa na tume hiyo.

Mwenyekiti wake, Jaji Joseph Warioba alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari, kwa lengo la kuwapa taarifa ya uendeshaji wa Mabaraza ya Katiba, ngazi ya serikali za mitaa ulivyofanyika.
Warioba alisema mikutano hiyo iliyoendeshwa na Tume ilianza Julai 12, 2013 na kumalizika Septemba 2, mwaka huu.
Alisema wakati Sheria Mama iliyoiunda Tume ya yake mwaka 2011 inatamka kwamba Tume iendelee kuwapo katika mchakato wote, hadi pale kura ya maoni ya kupitisha au kukataa Katiba mpya itakapofanyika.
Hata hivyo, alisema Muswada wa Sheria ya  Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2013 uliopitishwa katika mkutano wa Bunge wa 12, umekataa hilo.
Muswada huo uliungwa mkono na kupitishwa na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) na Augustine Mrema (TLP), lakini wabunge wa upinzani wa Chadema,CUF na NCCR-Mageuzi waliupinga na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge.
Jaji Wariona alisema marekebisho yaliyofanywa katika kikao cha 12 yanakinzana na Sheria mama kwa sababu, Muswada wa sasa unataja muda wa Tume kumalizika pale itakapowasilisha Rasimu ya Katiba, katika Bunge Maalum la Katiba.
“Tunajua kazi ya kutunga sheria si ya kwetu, ni ya wengine, na hata sheria inayotuongoza katika utendaji kazi wetu, tumeikuta ikiwa imeshatungwa tayari na wahusika, na hakika sisi tunafanya kazi kulingana na sheria iliyo mbele yetu,” alisema.
Jaji Warioba alisema hata hivyo kwamba, wakati Muswada wa Marekebisho unahitimisha ukomo wa Tume baada ya kuwasilisha Rasimu katika Bunge Maalumu la Katiba, Sheria mama inawataka waendelee mpaka kwenye hatua ya kura ya maoni.
Alisema Sheria mama inaitaka Tume iendelee mpaka kwenye hatua hiyo, ili pamoja na mambo mengine iweze kutoa elimu kwa wananchi.
“Sasa utafanya jukumu hilo kwa kutumia mamlaka ipi, wakati tayari shughuli zako zimefikia ukomo baada ya kuwasilisha Rasimu kwenye Bunge Maalum la Katiba?” alihoji Jaji Warioba.
KUJIUZULU WAJUMBE WA TUMEJaji Warioba alizungumzia pia taarifa zilizoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari za baadhi ya wajumbe wa Tume kutishia kujiuzulu kama ishara ya kupinga Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba uliopitishwa na Bunge hivi karibuni.
“Siyo kweli kuwa wanataka kujiuzulu. Kilichotokea ni kuwa baada ya safari ya kuzunguka karibu nchi nzima, na kukutana na changamoto nyingi ambazo ziliwachosha, zikiwemo za matamshi ya Kuwadhalilisha,” alisema.
Alisema baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa walitoa matamshi yaliyolenga kuwadhalilisha wajumbe wa Tume, na kuishusha thamani kazi iliyofanywa na Tume ya kuandika Rasimu ya Katiba.
“Aidha baadhi ya viongozi wa siasa pia walitoa matamshi yaliyowalenga wajumbe wa Tume, na kuwafanya baadhi ya wajumbe wa Mabaraza, kuwajadili wajumbe wa Tume, badala ya Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume,” alisema.
Hata hivyo, Jaji Warioba hakutoa maelezo zaidi kuhusiana na matamshi yaliyotolewa dhidi ya wajumbe wa Tume yake.
Alisema ni katika vikao vya kupitia safari hizo za wajumbe na changamoto walizokumbana nazo pamoja na uchovu waliokuwa nao kutokana na changamoto hizo, ndipo baadhi ya wajumbe walipoonekana kusema bwana basi, lakini hawakusema wanataka kujiuzulu.
Alisema Katiba inayotafutwa ni ile itakayoleta umoja wa Watanzania wote na ambayo itakuwa chachu ya maendeleo ya nchi kwa vizazi vijavyo.
“Hatutafuti katiba ya kundi moja au ya chama kimoja, au katiba itakayotokana na mapambano, kwa hiyo ni muhimu kwa viongozi wa kisiasa, wakaona busara ya kukaa pamoja na kuondoa tofauti zao,” alisema.
Jaji Warioba alisema, katiba yenye kuleta umoja haitapatikana kwa njia ya maandamano au malumbano ya kwenye majukwaa, na badala yake itapatikana kwa njia ya kuzimaliza tofauti walizonazo, kwa njia ya mazungumzo.
IDADI YA MIKUTANOIli kuendesha mikutano ya Mabaraza ya Katiba kwa ufanisi, Jaji Warioba alisema Tume ilijigawa katika makundi 14, kila kundi likiwa na wajumbe wawili au watatu.
Alisema makundi hayo yalizunguka nchi nzima na kufanya mikutano 179, iliyohudhuriwa na wajumbe 19,337, ambayo ilifanyika katika kila Halmashauri ya wilaya, Halmashauri ya Manispaa na jiji, huku mkutano mmoja ukidumu kwa wastani ya siku tatu.
Alisema jumla ya mikutano 166 ilifanyika Tanzania Bara na 13 ilifanyika Tanzania Zanzibar.
CHANGAMOTOAlisema baadhi ya changamoto zilizojitokeza ni za baadhi ya vyama vya siasa kuingilia uhuru wa wajumbe katika kutoa maoni yao kuhusu rasimu ya katiba.
Aidha, alizitaja zingine kuwa, ni kwenye baadhi ya maeneo, wajumbe wa Mabaraza ya Katiba walifundishwa nini cha kusema juu ya Rasimu ya Katiba, na baadhi ya vyama vya siasa kuendesha mikutano ya hadhara na ya ndani ya wanachama wao, sambamba na mikutano ya mabaraza.
KINACHOENDELEAJaji warioba alisema, kinachofanyika kwa sasa ni uchambuzi wa maoni yaliyotolewa na Mabaraza ya Katiba, kwa kufuata mwongozo ambao Tume imejiwekea na uchambuzi unafanywa kwa kuzingatia uzito wa hoja, zilizotolewa na wananchi katika maeneo tofauti ya Rasimu ya Katiba.
Alisema baada ya uchambuzi, Tume itaandaa Ripoti itakayojumuisha Rasimu ya Katiba iliyoboreshwa kutokana na maoni ya Mabaraza ya Katiba na kuiwasilisha kwa Rais wa Tanzania na wa Zanzibar, kama Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inavyolelekeza.
“Mipango ya Tume ni kukamilisha kazi hii ndani ya muda uliowekwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83,” alisema.
MJUMBE AITUMUMU CCMWakati Jaji Warioba akisema hayo, Mjumbe wa Tume hiyo, Dk. Sengondo Mvungi, amesema Chama Cha Mapinduzi)  kinaandaa rasimu yake ya Katiba Mpya, ili kiiwasilishe kinyemela kupitia kwa wabunge wake kwenye Bunge la Katiba litakalofanyika Novemba mwaka huu.
Alisema kuwa rasimu hiyo ni tofauti na  iliyotolewa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kwamba kutokana na hali hiyo, yuko  tayari kujiuzulu ujumbe katika tume hiyo ili kuepukana na aibu kutokana na CCM na serikali kuamua kuvuruga kwa makusudi mchakato wa kupata katiba mpya inayokidhi matakwa ya wananchi wote.
Aliliambia NIPASHE jana kuwa ni aibu kubwa kwa CCM kuamua kuandaa rasmu yake huku kikijua chombo kilichopewa mamlaka hayo ni Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kushiriki maadhimisho ya miaka 18 ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na kusema kuwa anazo taarifa za uhakika kwamba mpango huo wa CCM umeandaliwa na makada wa chama na umeishakamilika hivi sasa.
Dk. Mvungi alisema CCM kimemaliza kuandaa rasimu hiyo na kwamba kitaiwasilisha katika Bunge la Katiba na wabunge wake wamejipanga kuitetea mpaka ipite.
Alisema hali ni mbaya kwa tume kwa kuwa imeingiliwa na CCM na serikali yake na kwamba mambo yakiendelea hivyo, wake watajiondoa.
Amesema kwa upande wake yupo tayari kujiuzulu na kukaa pembeni badala ya kuendelea kupata aibu huku Watanzania wakimtazama.
“Mimi nipo tayari, nasubiri wajumbe wenzangu, wakisema kujiondoe hata sasa mimi nipo tayari kufanya hivyo kwa kuwa sikuingia kule kutafuta fedha, bali kuwawakilisha wananchi,” alisema Dk. Mvungi
“Aina ya sasa iliyotumika kuandika Katiba hii imewachanganya CCM na serikali na sasa wameamua kuvuruga mchakato kwa makusudi,” aliongeza Dk. Mvungi.
Alitaja mambo matatu ambayo yanaichangana CCM na serikali ni pamoja na rasimu hiyo kutamka suala la kuwapo serikali tatu, mbunge kuwekewa ukomo wa vipindi  vitatu vya miaka 15 na wabunge kutokuwa mawaziri.
KAULI YA MANGULAAkizungumzia tuhuma hizo, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula, alikanusha na kusema siyo za kweli.
Mangula baada ya kupokea simu jana jioni alisema alikuwa kwenye kikao Bagamoyo mkoani Pwani.
MAALIM SEIF: JK USISAINIMakamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hmad, amemuomba Rais Jakaya Kikwete kutousaini muswada huo badala yake ufanyiwe kwanza marekebisho.
Maalim Seif alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na Wazanzibari wanaoishi Tanzania Bara na kufafanua kuwa Wazanzibar hawakushirikishwa katika kutoa maoni.
Aidha, alisema Rasimu ya Katiba mpya inapaswa kutamka Serikali ya Tanganyika badala ya Tanzania Bara katika mfumo wa Muungano wa serikali tatu za  Zanzibar, Tanganyika na Shirikisho.
Imeandikwa na Raphael Kibiriti, Richard Makore na Muhibu Said.

mbowe nae anena mazito khus katiba



Mbowe: Katiba Mpya inahitaji hekima, busara

“Hebu angalieni sasa hivi kuna ugomvi wa dini, wananchi na Serikali hususan katika maeneo yaliyo na madini, vyombo vya usalama na raia na mengine mengi. Je hii ndiyo Tanzania yenye amani na mshikamano aliyoiacha Hayati Baba wa Taifa?” Mbowe 

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema, kukusanya maoni ya wananchi kwa ajili ya kupata Katiba Mpya siyo kazi rahisi, ni kazi inayohitaji nia ya dhati ya taifa zima, kwa kuwa katiba ni mali ya wananchi na rasilimali za taifa.Mbowe alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wa hadhara wa kukujadili Rasimu ya Maoni ya Katiba, uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo wilayani Musoma Mkoa wa Mara hivi karibuni.
Alisema kwa kutambua umuhimu wa kazi hiyo, Chadema wameamua kuzunguka nchi nzima kwa lengo la kutoa elimu ya Katiba kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na kutoa ufafanuzi wa maana ya Katiba na kujibu hoja za wananchi hao.
Alisema kuwa Tanzania ambayo ilikuwa ikisifika kama nchi ya amani na mshikamano kwa miaka mingi, sasa inaelekea kubomoka na hali hiyo inatokana na katiba mbovu isiyokuwa na mipaka ya madaraka ambayo sasa tumeamua kuifanyia mabadiliko.
“Hebu angalieni sasa hivi kuna ugomvi wa dini, wananchi na Serikali hususan katika maeneo yaliyo na madini, vyombo vya usalama na raia na mengine mengi. Je hii ndiyo Tanzania yenye amani na mshikamano aliyoiacha Hayati Baba wa Taifa?” alihoji Mbowe.
Alisema katika kuzungumzia Katiba hakuna vyama vya siasa, polisi wala mtu wa kada nyingine yoyote. Katiba ni mali ya Watanzania wote, hivyo kila mmoja ana wajibu wa kutoa maoni yake juu ya mambo anayoamini kuwa yatalisaidia taifa kama yataingizwa kwenye katiba.
Awali akihutubia katika mkutano huo,Mmbunge wa Ubungo John Mnyika, alisema kuwa maadili ya uongozi na utawala bora, vinatikiswa kama siyo kuyumbishwa. Aliwataka wananchi kuhakikisha misingi ya taifa inarekebika kupitia marekebisho ya katiba mpya.
Mnyika alisema kuwa katika kupitisha maoni ya katiba, wanataka haki, uwazi na usawa katika masuala ya madini na rasilimali za nchi ambazo kimsingi zinapaswa kutajwa kwenye katiba. Tunataka Katiba pia impunguzie rais madaraka, alisema.
Alisema gharama za maisha ya wananchi zinazidi kupanda kila kukicha kutokana na rais kuwa na mlimbikano wa madaraka, hivyo kufanya maamuzi bila kutambua kuwa wananchi walio na kima cha chini ndio wanaoumia.
Aidha alisema kuwa anashangazwa na serikali ya CCM inavyokataa mfumo wa serikali tatu kwa madai kuwa,serikali tatu ni gharama kubwa sana kuendesha huku wakisahau baraza kubwa la mawaziri lisilo na meno.
Chadema imekuwa ikifanya mikutano ya hadharani nchini kuzungumzia mchakato wa katiba. Wamekuwa wakitoa elimu na kuwaeleza wananchi umuhimu wa kazi hiyo kwa taifa.

Nyie ni watu wabaya

 Mtoto wa miaka 4 awaambia magaidi



  • Magaidi walionekana kuumizwa na kauli za mtoto aliyewaambia kuwa wao ni watu wabaya, wakamwomba msamaha na kumpa chokleti.


Mtoto wa miaka minne ambaye ni raia wa Uingereza, Elliott Prior ameonyesha ushujaa wa hali ya juu baada ya kuweza kuwatolea maneno makali na ya kugusa magaidi waliovamia jengo la maduka la Westgate.Baada ya maneno hayo, baadhi ya taarifa zilizochapishwa kwenye vyombo mbalimbali vya kimataifa, vinasema magaidi hao waliomba mtoto huyo awasamehe kwa maelezo kuwa wao siyo watu wabaya.
Inaelezwa kuwa, kitendo cha mtoto huyo kilikuwa cha kishujaa kwani aliweza kuwaeleza magaidi hao maneno hayo, bila kuogopa silaha nzito walizokuwa wameshika mkononi huku baadhi ya watu wakiwa wameshauuawa.
Mtandao wa Daily Mail unasema mtoto huyo alimwambia mmoja wa magaini hao kuwa ‘Nyie ni watu wabaya sana’.
Mtandao huo unasema mtoto huyo aliyasema maneno hayo kama njia ya kumkinga mama yake Amber, aliyekuwa amepigwa risasi mguuni pamoja na dada yake Amelie, mwenye umri wa miaka sita ambaye walikuwa wote ndani ya duka hilo.
Katika kile kilichotafsiriwa kuwa ni kuumizwa na maneno hayo, magaidi hao walimpa Elliott pamoja na dada yake mifuko miwili miwili ya chokleti na kuwaomba msamaha.
Taarifa hizo zinasema kuwa,  gaidi huyo alisema “Samahani nisamehe, sisi siyo watu wabaya”.
Mama huyo anasema kuwa, kabla ya kukamatwa na magaidi hao, yeye na watoto wake walikuwa wamejificha kwenye jokofu la kuhifadhi nyama lililopo ndani ya duka la Nakumatt kwa zaidi ya saa moja na  nusu.
Anasema kuwa, baada ya kukamatwa na magaidi hayo, walimpiga risasi ya paja.
Mjomba wa watoto hao aliliambia gazeti la The Sun la Uingereza kuwa  “Walikuwa na bahati kuweza kutoka kwenye mikono ya hao magaidi. Hao magaidi walisema kuwa, kama kuna mtoto yeyote aliye hai ndani ya jengo hilo wanaweza kuondoka.
‘Mama yao alisimama na kusema ‘ndio’ , binamu yangu aliweza kupata ujasiri wa kusimama na kuwaambia kuwa, nyie ni watu wabaya sana’.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, baada ya magaidi hao kujua kuwa mama huyo na watoto wake hawakuwa kati ya watu waliowalenga, hawakuwaua.


Abdul Haji:Mkenya aliyekuwa tayari kuuawa


Abdul Haji akimwokoa mtoto asiuawe na magaidi. Picha ya maktaba 


Wakati vyombo vya usalama vya Kenya vikitangaza kulidhibiti jengo lote la Westgate lililovamiwa na magaidi wanaodaiwa kuwa wa kundi la Al-Shabaab, baadhi ya watu waliojitoa muhanga na kufanikiwa kuokoa maisha ya wengine, wanaendelea kuibuka.Hivi karibuni gazeti hili lilichapisha habari juu ya askari wa Kikosi Maalumu cha Anga (SAS) cha Uingereza, aliyeweza kuokoa zaidi ya watu 100 ndani ya jengo hilo.
Hivi karibu, baadhi ya vyombo vya habari vya Kenya vimemnukuu pia  Abdul Haji (38) ambaye ni raia wa kawaida aliyeweza kufika ndani ya jingo hilo na kuokoa watu waliokuwa wametekwa na wanamgambo hao wanaodaiwa kuwa wa Al Shabaab.
Gazeti la Daily Nation, limemnukuu kijana huyo akisema alipata ujumbe mfupi wa simu ya mkononi (SMS) kutoka kwa kaka yake ukisomeka kuwa “Nimekwamba Westgate, nadhani kuna magaidi wamevamia hapa, niombee”.
Kijana huyo ambaye asili yake ni Msomali, alisema alipata sana hofu kutokana na ujumbe huo wa kaka yake kwani ilikuwa ni wiki mbili tu tangu televisheni moja ya nchi hiyo kumtaja kaka yake huyo kama mmoja wa watu anaowasaidia magaidi hao wa Al Shabaab.
Kijana huyo ambaye ni mtoto wa Seneta, Yusuf Haji alisema hali hiyo ilimpa wasiwasi zaidi kwani tayari walishaanza kupata vitisho kutoka kwa baadhi ya watu wakiamini kuwa kweli familia yake wanawasaidia Al Shabaab.
Anasema baada ya ujumbe huo alikimbia mara moja na kwenda katika jengo hilo la Westgate, na muda mfupi tu tangu magaidi hao kuingia ndani ya jengo hilo na kuanza kuwafetulia watu risasi alikuwa ameshawasili eneo hilo.
Haji ambaye ni mfanyabishara na baba wa watoto wane wa kike, alisema aliamini kuwa magaidi hao walikuja kumfuata kaka yake na baadaye familia nzima hivyo aliamua kujitoa muhanga ili kumuokoa kaka yake na familia yake yote.
Mtoto huyo ambaye baba yake ni Seneta wa Garissa na aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ulinzi wan chi hiyo, alisema aliingia kwenye jengo hilo akiwa na bastola ambayo anaimiliki kwa kufuata sheria zote za Kenya.
Anasema kuwa, alipofika ndani ya jengo hilo aliona watu wengi wakiwa wameuwawa wakiwa wamelala chini na wengine wakiwa bado wapo hai huku milio ya risasi ikiendelea kulia kila kona.
Aliungana na watu wengine kama 10 waliokuwa ndani ya jengo hilo ambao pia walikuwa na silaha ili waone namna  ya kusaidia baadhi ya watu.
 “Nimewahi kuona miili ya watu waliokufa lakini sijawahi kuiona mingi kama ile ikiwamo ya watoto na kinamama wasiojiweza,” anasema Haji

Warioba: nae izungumzia kuhus katba

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu, Joseph Warioba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Makamu wake, Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani. Picha na Fidelis Felix 

*******************************************************************************************************************************************************************

Dar es Salaam. Wakati wananchi wa kada mbalimbali wakishinikiza Rais Jakaya Kikwete kutokusaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba 2013, kwa maelezo kuwa una kasoro, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba naye amesema sheria ina upungufu.

Warioba alisema jana kwamba ni jambo la kushangaza sheria hiyo kueleza kuwa tume hiyo itavunjwa baada ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalumu la Katiba, wakati huohuo ikieleza kuwa itahusika tena kusimamia utoaji wa elimu ya kura ya maoni.

Kauli hiyo ya Warioba imekuja wakati vyama vya NCCR Mageuzi, Chadema na CUF, vikifanya mikutano nchi nzima kuwashawishi wananchi kupinga kile wanachokiita hujuma dhidi ya upatikanaji wa Katiba Mpya.
Muswada huo ulipitishwa na wabunge wa CCM baada ya wale wa upinzani kutoka nje baada ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe kuamuriwa na Naibu Spika, Job Ndugai kutoka nje kutokana na kukaidi kwake amri ya kukaa chini alipokuwa akitaka kutoa hoja kabla ya mjadala wake kuanza.
Muswada huo unapingwa kwa kuwa Rais amepewa mamlaka ya kuteua wajumbe 166, ambao si wabunge wala wawakilishi na Zanzibar kutokushirikishwa kikamilifu kwenye maandalizi ya muswada huo.
Alisema baada ya kuipata sheria hiyo: “Tulijiuliza maswali kwa sababu miswada huwa inapelekwa bungeni na Serikali ikiwemo ya Katiba. Anayeipeleka kama ni waziri ndiye anayetoa ufafanuzi pale inapohitajika.”

Sheria hiyo ambayo Warioba amesema ina upungufu, muswada wa marekebisho yake ulijadiliwa na kupitishwa wa wabunge Septemba 6, mwaka huu katika Mkutano wa 12 wa Bunge Mjini Dodoma, ikiwa ni baada ya kubadilishwa kwa baadhi ya vifungu na hivi sasa Rais Kikwete anasubiriwa kuusaini ili iwe sheria kamili. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Jaji Warioba alisema: “Mwisho wa kazi ya tume ni baada ya kukabidhi rasimu, hilo ni tatizo. Maana tume itakuwa imeshavunjwa, sasa itafanyaje kazi ya kutoa elimu kwenye kura ya maoni?”

Jaji Warioba pamoja na kukiri upungufu huo, alisema kurekebisha au kutokurekebisha kasoro hizo si jukumu la tume hiyo.

“Tunawaomba watafakari, waone jinsi gani tume ambayo imekwishavunjwa itakuja kutoa elimu wakati wa kura ya maoni, sheria ina ‘contradiction’ (ina mkanganyiko),” alisema.

Hata hivyo, Warioba alisema pamoja na kasoro hizo Tume hiyo inafanya kazi yake kwa kufuata sheria hiyo huku akisisitiza, “Wanaotunga sheria ni wengine siyo sisi, tulipoteuliwa tulikuta sheria na kuanza kazi kwa kuifuata. Imefanyiwa marekebisho sisi tunafuata.”

Alisema waliofanya mabadiliko ya sheria hiyo wana haki ya kufanya hivyo na kwamba Tume ya Mabadiliko ya Katiba haiwezi kuzuia kutokufanyika kwa mabadiliko hayo, kwani yapo baadhi yanaihusu.

Alisema kulingana na sheria, tume yake ndiyo inayotakiwa kutoa ufafanuzi katika Bunge la Katiba, kama ambavyo Waziri hutoa maelezo anapowasilisha muswada bungeni.

Katiba mpya Tanzani bado majanga kwa vyama pinzani

Katiba mpya Tanzani bado majanga kwa vyama pinzani

Prof Ibrahimu Lipumba

Chama cha Wananchi (CUF) kimesema kinaungana na Watanzania walioonyesha shaka juu ya mchakato wa kupata Katiba mpya kwani hakioni nia njema na utayari wa Tume kuwa na Katiba inayotokana na maoni ya wananchi.

Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Irahim Lipumba, alisema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maazimio ya kikao cha baraza kuu la chama hicho kitaifa.


Alitaka  Rasimu ya Katiba inayoandaliwa iwekwe hadharani kwa wakati ili wananchi waweze kutoa maoni yao kabla haijapelekwa katika Bunge la Katiba na kupigiwa kuwa na wananchi.

Alisema Cuf hakitakuwa tayari kuiunga mkono Katiba ambayo haitakuwa na misingi imara ya kidemokrasia na isiyotokana na maoni ya Watanzania na kitakuwa tayari kuwahamasisha kuikataa katiba hiyo.

Profesa Lipumba ameitaka tume ya kuratibu ukusanyaji wa maoni kuweka mpango wa kuyafikia makundi yenye mahitaji maalumu ikiwa ni wanawake, walemavu, vijana na asasi za kiraia zinazoshughulika na malezi ya watoto ili yaweze kutoa maoni yao.

Alisema pamoja na mchakato wa uandikaji wa katiba kupangiwa miezi 18 muda huo  hautoshi  kwani kuna chaguzi mbalimbali ambazo zinatarajiwa kufanyika mwakani hivyo hakuna sababu za msingi za kuharakisha zoezi hilo na kupata katiba mbovu isiyokidhi matakwa ya wananchi na badala yake kupata katiba ya matakwa ya kikundi kidogo cha watu wenye dhamana.

hata hivyo prfesa lipumba amewataka wananchi wasipelekwe pelekwe tu kama gari bovu na wala wasifuate upepo kama bendera amesema nilazima wananchi washirikishwe kikamailifu ili ipatikane katiba bora na yenye tija, ametaka na watu wa wazenjibari nawao washirikishwe na akamalizia kwa kusema kua kila mtanzania ana haki ya kutoa ushauri juu ya mchakato wa katiba mpya.