TANGAZO

TANGAZO
WEKA TANGAZO LAKO HAPA

Jumamosi, 5 Oktoba 2013

Watu wanne wauwawa Mombasa

Kenya

Watu wanne wamethibitishwa kuuwawa baada ya makabiliano makali kati ya polisi na waandamanaji mjini Mombasa kenya walioandamana hapo jana baada ya Sala ya Ijumaa kupinga kuuwawa kwa Sheikh Ibrahim Ismail
.

 Sheikh Ibrahim aliuwawa kwa kumiminiwa risasi siku ya Alhamisi usiku pamoja na wenzake watatu walipokuwa katika gari  wakielekea nyumbani. Katika maandamano hayo kanisa moja lilichomwa moto.

 Kulingana na shirika la msalaba mwekundu watu wanne waliouwawa wote walikuwa na majeraha ya risasi walioyapata walipokuwa wanakabiliana na polisi.

 Sheikh huyo anaaminika kuhubiri katika msikiti Musa mjini humo unaoaminika kuwa na mafungamano na kundi la kigaidi la Al shabaab, walioshambulia jengo la Westgate mjini Nairobi wiki mbili zilizopita na kusababisha mauaji ya watu 67.

 Hata hivyo hakuna kundi lolote au mtu yeyote aliyekiri kuhusika na mauaji ya sheikh Ibrahim na wenzake.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni