Zaidi ya watu miamoja kumi na watu wamepatikana wakiwa wamekufa maji na wengine miambili bado hawajulikani waliko
Hali mbaya ya hewa imewasababisha waokoaji kuahirisha juhudi za kutafuta miili ya wahamiaji zaidi ya 200 ambao hawajulikani waliko, baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kushika moto na kuzama karibu na kisiwa cha Lampedusa, kusini mwa Italia. Wapiga mbizi walifanikiwa kuipata miili zaidi ya 100 ya wahamiaji huku watu zaidi ya 150 wameokolewa. Inaaminika boti hiyo iliopinduka ilikuwa na wahamiaji takriban 500 waliokuwa wanatokea nchini Somalia na Eritrea. Kamishna wa Umoja wa Ulaya anayeshughulika na maswala ya ndani Cecilia Malmstroem, ameapa kuwa atapambana na watu wanaosafirisha watu kwa njia haramu kwa kutumia hali yao mbali ya maisha. Italia ilitangaza siku moja ya maombolezo jana Ijumaa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni