Malaki ya waumini wamekusanyika Mina karibu na mji wa Saud Arabia wa Makka kuanza kutekeleza nguzo ya tano ya dini ya kiislam-Hajji.
Kawaida waumini hupitisha usiku kucha ndani ya mahema katika eneo hilo kabla ya kuelekea katika mlima
Arafat kesho jumatatu.Kabla ya hapo waumini wa dini ya kiislam walifanya ibada yao kwa kuizunguka Kaaba iliyoko ndani ya msikiti mkubwa wa Makka.
Hajji ya mwaka huu itakamilika ijumaa ijayo.Askari polisi na wanajeshi zaidi ya laki moja walmewekwa kuhakikisha
Hajji inafanyika bila ya shida.Kwa mujibu wa dini ya kiislam,kila muislam mwenye kujiweza anatakiwa angalao mara moja katika maisha yake akahiji Makka-mji alikozaliwa Mtume Muhammad.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni