TANGAZO

TANGAZO
WEKA TANGAZO LAKO HAPA

Jumanne, 1 Oktoba 2013

Mapigano makali yaendelea mashariki mwa Kongo




Mapigano makali yaendelea mashariki mwa Kongo

Kwa akali watu 10 wameuawa na makumi  ya wengine kujeruhiwa baada ya kujiri mapigano makali kati ya wapiganaji wa kundi la Alliance of Patriots for a Free and Sovereign Congo  APCLS na wanamgambo wa kundi la Sheka katika eneo la Kalembe mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Taarifa zinasema kuwa, mapigano hayo yametokea umbali wa kilomita 90 kaskazini magharibi mwa mji wa Goma, makao makuu ya jimbo la Kivu Kaskazini. John Banyene, kiongozi wa asasi ya kijamii katika eneo hilo amesema kuwa, kwa akali watu 16 wameuawa kwenye mapigano hayo, wakiwemo raia kadhaa.  Kwa miezi kadhaa sasa eneo la mashariki mwa Kongo limegeuka kuwa uwanja wa mapigano kati ya makundi mbalimbali ya waasi dhidi ya vikosi vya jeshi la nchi hiyo. Umoja wa Mataifa na hata serikali ya Kongo zimekuwa zikiituhumu Rwanda kuwa inawaunga mkono waasi wa eneo hilo, tuhuma ambazo zimekanushwa vikali na serikali ya Kigali.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni