10 wafariki katika ajali ya moto ndani ya hospitali Japan
Watu kumi wamethibitishwa kufa baada ya moto kuzuka katika hospitali moja mapema leo katika mji wa Kusini mwa Japan, Fukuoka.
Waathiriwa hao wanaaminika kuwa wagonjwa wanane na wafanyakazi wawili.
Watu wengine watano wamejeruhiwa, kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kyodo ambalo liliwanukuu polisi.
Wakati moto huo ulipozuka, jumla ya watu 17 walikuwemo ndani ya hospitali hiyo yenye ghorofa 4 na wawili kati yao walisalimika. Inasemekana moto huo ulianza katika chumba kimoja cha matibabu katika ghorofa ya chini.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni