Ripoti mpya iliyotolewa na Umoja wa Mataifa imesema kuwa idadi ya watu wanaokimbia vita na machafuko katika Jamhuri ya Kidemokrasia ay Congo imeongezeka na kuwa zaidi ya laki tatu na nusu katika miezi ya hivi karibuni.
Ripoti iliyotolewa jana na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ilisema kuwa mwishoni mwa mwezi wa Agosti karibu Wacongo laki 4 na elfu 40 walikimbia vita na kuingia katika nchi jirani za Burundi, Rwanda na Uganda.
Ripoti zinasema tangu mwezi Mei mwaka 2012 yapata wakimbizi milioni tatu wamekimbia nyumba zao huko mashariki mwa Congo. Milioni mbili na nusu kati yao wamekimbilia ndani ya nchi hiyo na karibu laki tano wameomba hifadhi katika nchi jirani.
Jeshi la Congo likisaidiwa na askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa linapambana na waasi wa kundi la M23. Mapigano mengine mapya yamezuka kati ya wapiganaji wa kundi la Alliance of Patriots for a Free and Sovereign Congo (APCLS) na wanamgambo wa kundi la Sheka katika eneo la Kalembe huko mashariki mwa Congo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni