Jeshi la Rwanda limekosoa vikali vikwazo vilivyowekwa na Marekani dhidi ya nchi hiyo. Taarifa zinasema kuwa, Marekani imechukua uamuzi huo baada ya kulituhumu jeshi la Rwanda kuwa liliwasaidia waasi wa M23 wa Kongo katika kuwatumikisha watoto jeshini.
Joseph Nzabamwita, Msemaji wa Jeshi la Rwanda amesema kuwa tuhuma hizo za Washington hazina ukweli, na wala hazina ushahidi wowote. Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani imetangaza kuwa, nchi hiyo imesimamisha misaada ya kifedha na kijeshi kwa nchi hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2014, kuanzia tarehe mosi Oktoba mwaka huu.
Wakati huohuo, ujumbe wa wataalamu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa umeelekea katika eneo la ukanda wa Maziwa Makuu ya Afrika kwa shabaha ya kutoa msukumo wa usalama na amani katika eneo hilo. Taarifa ya Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa, ujumbe huo utakutana na marais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda, Uganda na Waziri Mkuu wa Ethiopia.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni