Rais wa Marekani Barrack Obama amefuta ziara yake barani Asia na pia hatohudhuria mikutano miwili ya kimataifa kutokana na kufungwa kwa shughuli za serikali ya Marekani.
Shughuli za baadhi ya ofisi za serikali ya Marekani zilifungwa siku ya Jumanne kufuatia bunge la la nchi hiyo kushindwa kufikia makubaliano juu ya bajeti mpya.
Warepublikan ambao wanadhibiti sehemu kubwa ya baraza la wawakilishi wanataka kucheleweshwa kwa mpango wa rais Obama wa kutoa huduma ya afya ujulikanao kama Obamacare.
Wabunge hao wa Republican wanashinikiza sheria hiyo ya mabadiliko ya afya iondolewe au mpango huo hautapokea fedha za kuugharamia.
Hata hivyo wabunge wa chama cha Demokratic na wale wa Republikan kwa sasa hawaonekani kuwa katika njia moja ya kusuluhisha tofauti zao.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni