Watu watatu akiwemo msichana mdogo mwenye umri wa miaka 8 aliuawa wakati watu waliokuwa wamejihami wakiwa kwenye pikipiki kushambulia sherehe za ndoa nje ya kanisa la Kikopti mjini Cairo.
Mabaki ya magari ya madereva waliouawa na Boko Haram
Wanamgambo waliokuwa wamevaa nguo za kijeshi, wamewaua watu 19 katika kuzuizi cha barabarani walichokuwa wameweka kukagua magari katika jimbo la Borno.
Jamani waislamu tusipelekwe tu kama magari mabovu na hawa bakwata kwasababu sijui niwaweke katika kundi gani yaani hawana hata aibu wanatangaza edd jumatano haliya kua watu wana simama arafa kesho waislamu tuamke tuacheni kulala jamani. hii ndo taarifa yao hebu isome. chanzo bakwata.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ametengua maamuzi yaliyofanywa na Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli ya kuongeza tozo ya asilimia tano kwa wasafirishaji wa malori na mabasi kwa uzito unaozidi.
Wakenya wameghadhabishwa sana na hatua ya wanaume watatu waliombaka msichana mmoja na kutupa mwili wake kwenye choo kuamrishwa na polisi kukata nyasi kama adhabu kwao.
Rais Banda amewafuta kazi mawaziri wake wote kutokana na ufisadi
Rais wa Malawi, Joyce Banda amelifuta kazi baraza lake la mawaziri kutokana na kuongezeka kwa visa vya ufisadi serikalini.
Maafisa wa serikali wamekuwa wakipatikana na pesa zikiwa zimefichwa chini ya vitanda vyao na kwenye magari yao, kwa mujibu wa mwandishi wa BBC Raphael Tenthani.
Taliban wako tayari kwa mazungumzo ila wataendelea kushambulia maslahi ya Marekani
Kiongozi wa Taliban nchini Pakistan Hakimullah Mehsud ameambia BBC kuwa yuko tayari kwa mazungumzo na serikali ingawa amesisitiza kuwa bado serikali haijamshauri.
Wapiga mbizi nchini Utaliana wamapeta idadi kubwa ya maiti katika boti iliyozama na ambayo ilikua imewabeba wahamiaji wa kiafrika kwenda Ulaya siku ya Alhamisi.
Serikali ya Kenya imetaja majina ya watu 4 waliofanya shambulizi la kigaidi kwenye jengo la kibiashara la Westgate mjini Nairobi, na kutoa picha za video zinazowaonyesha magaidi hao ndani ya jengo walilolishambulia.
Mtafaruku ndani ya jengo la Westgate siku ya mashambulizi
MTOTO WA AJABU AZALIWA ZANZIBAR, AANZA KUONGEA AKIWA NA MIEZI MIWILI TU. MAMA AMFIKISHA KWA VIONGOZI NA KUFUNGUKA MAKUBWA. SOMA HAPA
MTOTO wa miezi 10, aliyetambuliwa kwa jina la Fahazal mkazi wa Kivunge amefikishwa mbele ya serikali ya mkoa wa kaskazini Unguja, baada ya mama yake mzazi kusema amekuwa akitokewa na maajabu na kwamba jamii iombe dua ili kunusuru kutokea vifo.
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho, jijini Dar es Salaam, jana. PICHA | FIDELIS FELIX
Dar es Salaam.
Siku sita baada ya Serikali kuyafungia magazeti ya Mwananchi na Mtanzania kwa madai ya
Rais wa Marekani Barrack Obama amefuta ziara yake barani Asia na pia hatohudhuria mikutano miwili ya kimataifa kutokana na kufungwa kwa shughuli za serikali ya Marekani.
Watu wanne wamethibitishwa kuuwawa baada ya makabiliano makali kati ya polisi na waandamanaji mjini Mombasa kenya walioandamana hapo jana baada ya Sala ya Ijumaa kupinga kuuwawa kwa Sheikh Ibrahim Ismail
Zaidi ya watu miamoja kumi na watu wamepatikana wakiwa wamekufa maji na wengine miambili bado hawajulikani waliko
Hali mbaya ya hewa imewasababisha waokoaji kuahirisha juhudi za kutafuta miili ya wahamiaji zaidi ya 200 ambao hawajulikani waliko, baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kushika moto na kuzama karibu na kisiwa cha Lampedusa, kusini mwa Italia. Wapiga mbizi walifanikiwa kuipata miili zaidi ya 100 ya wahamiaji huku watu zaidi ya 150 wameokolewa. Inaaminika boti hiyo iliopinduka ilikuwa na wahamiaji takriban 500 waliokuwa wanatokea nchini Somalia na Eritrea. Kamishna wa Umoja wa Ulaya anayeshughulika na maswala ya ndani Cecilia Malmstroem, ameapa kuwa atapambana na watu wanaosafirisha watu kwa njia haramu kwa kutumia hali yao mbali ya maisha. Italia ilitangaza siku moja ya maombolezo jana Ijumaa.
Idadi kubwa ya wafuasi wa Morsi wamezuiliwa na wengine kuuawa
Vikosi vya usalama nchini Misri vimeimarisha ulinzi katika sehemu kadhaa mjini Cairo baada ya vurugu kuzuka kutokana na makabiliano kati ya wafuasi wa Mohammed Morsi na vikosi vya usalama katika mji huo na ule wa Alexandria.
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ametangaza kuwa mgogoro baina ya Tanzania na Rwanda umemalizika.
Katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi kwa raia wa nchi hiyo Rais Kikwete amesema hatua hiyo inafuatia mazunguzo baina ya viongozi hao wawili yaliyofanyika hivi karibuni nchini Uganda
Jeshi la Rwanda limekosoa vikali vikwazo vilivyowekwa na Marekani dhidi ya nchi hiyo. Taarifa zinasema kuwa, Marekani imechukua uamuzi huo baada ya kulituhumu jeshi la Rwanda kuwa liliwasaidia waasi wa M23 wa Kongo katika kuwatumikisha watoto jeshini.
Baadhi ya waliopoteza maisha yao wakitafuta kuingia Ulaya
Juhudu za uokozi zimeanza tena Kusini mwa Utaliano baada ya boti iliyokuwa imewabeba wahamiaji wa kiafrika kwenda Italia, kuzama katika kisiwa cha Lampedusa.
Duru ya kwanza ya mazungumzo ya moja kwa moja kati ya chama tawala cha an Nahdha nchini Tunisia na vile vya upinzani yenye lengo la kutatua mivutano ya kisiasa, itaanza hapo kesho nchini humo
Jimbo la Niedersachsen moja kati ya majimbo 16 nchini Ujerumani, limeitambua dini ya Kiislamu kuwa ni dini rasmi kwenye jimbo hilo lililoko kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
Mahakama ya kimataifa ya ICC, imetoa kibali cha kukamatwa kwa raia Mkenya ambaye anatuhumiwa kwa kujaribu kuwahonga mashahidi ili wajiondoe kwenye kesi dhidi ya Naibu Rais wa Kenya William Ruto.
Bwana Ble anashukiwa kufanya mauaji, ubakaji, mateso na vitendo vingine vya kinyama
Mahakama ya kimataifa ya ICC, imetangaza rasmi kutoa kibali cha kumkamata aliyekuwa waziri wa Ivory Coast,Charles Ble Goude kwa madai ya uhalifu wa kivita
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta atoa Onyo kali kwa magaidi
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa majeshi ya Kenya yataendelea kukaa Somalia hadi usalama utakapoimarishwa katika nchi hiyo iliyokumbwa na vita vya miaka mingi.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa viongozi wa Marekani wanapaswa kuamiliana na Iran kwa kutilia maanani uhakika wa mambo na kuliheshimu taifa la nchi hii
Ripoti mpya iliyotolewa na Umoja wa Mataifa imesema kuwa idadi ya watu wanaokimbia vita na machafuko katika Jamhuri ya Kidemokrasia ay Congo imeongezeka na kuwa zaidi ya laki tatu na nusu katika miezi ya hivi karibuni.
Kwa akali watu 10 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa baada ya kujiri mapigano makali kati ya wapiganaji wa kundi la Alliance of Patriots for a Free and Sovereign Congo APCLS na wanamgambo wa kundi la Sheka katika eneo la Kalembe mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.