TANGAZO

TANGAZO
WEKA TANGAZO LAKO HAPA

Ijumaa, 27 Septemba 2013

Polisi ya Kimataifa yaanza msako Kenya

Polisi ya Kimataifa yaanza msako Kenya

Polisi ya  kimataifa Interpol, imeanza msako leo dhidi ya mwanamke wa Kiingereza aliyepewa jina la “  Mjane mweupe” baada ya kutolewa  waranti wa kukamatwa kufuatia shambulizi la kigaidi katika jengo la kibiashara la Westgate  katika mji mkuu wa Kenya Nairobi. Samantha Lewthwaite aliyesilimu na mwenye umri wa miaka 29 aliolewa na Germaine Lindsay mmoja wa  washambuliaji wanne Wakiislamu waliojiripua kwa mabomu walipoushambulia mtandao wa usafiri wa chini ya ardhi mjini London Julai 7 mwaka  2005 na kuwauwa watu  52.Polisi ya kimataifa imesema mwanamke huyo, mama wa watoto watatu, anatakiwa na Kenya kujibu mashitaka ya kumiliki miripuko na kula njama ya kufanya hujuma  tangu Desemba 2001. Awali Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Kenya Amina Mohammed alisema mwanamke  mmoja wa Kiingereza alikuwa mmoja wa washambuliaji, ingawa Rais Uhuru Kenyatta alisema baadae kwamvba ripoti hizo hazikuthibitishwa. Wizara ya kigeni ya Uingereza na polisi ya nchi hiyo imekataa kusema lolote, ikisisitiza kwamba hilo ni suala la polisi ya  kimataifa na maafisa wa Kenya.

Alhamisi, 26 Septemba 2013

dua mbalimbali

Dua
Jumapili, 18 Machi 2012 18:53

Dua baada ya Sala ya Isha

بسم الله الرحمن الرحیم اَللّهُمَّ اِنَّهُ لَيْسَ لي عِلْمٌ بِمَوْضِعِ رِزْقي وَاِنَّما اَطْلُبُهُ بِخَطَرات تَخْطُرُ عَلى قَلْبي فَاَجُولُ فى طَلَبِهِ الْبُلْدانَ فَاَنَا فيما اَنَا طالِبٌ كَالْحَيْرانِ لا اَدْري اَفى سَهْل …
Jumapili, 18 Machi 2012 18:52

Dua baada ya Sala ya Magharibi

بسم الله الرحمن الرحیم اَللّهُمَّ اِنّي أَسْأَلُكَ مُوجِباتِ رَحْمَتِكَ وَعَزائِمِ مَغْفِرَتِكَ وَالنَّجاةُ مِنَ النّارِ وَمِنْ كُلِّ بِلِيَّة وَالْفَوْزَ بِالْجَنَّةِ وَالرِّضْوانِ في دارِ السَّلامِ وَجَوارِ نَبِيِّكَ مُحَمَّد عَلَيْهِ وَآلِهِ اَلسَّلامُ اَللّهُمَّ …
Jumapili, 18 Machi 2012 18:29

Dua ya baada ya Sala ya Alasiri

بسم الله الرحمن الرحیم اَسْتَغْفِرُ اللهَ الَّذي لا اِلهَ اِلاّ هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ الرَّحْمنُ الرَّحيمُ ذُو الْجَلالِ وَالاِْكْرامِ وَأَسْأَلُهُ اَنْ يَتُوبَ عَلَيَّ تَوْبَةَ عَبْدٍٍِِ ذَليل خاضِع فَقير بائِس مِسْكين مُسْتَكين …
Jumapili, 18 Machi 2012 18:22

Dua baada ya Sala ya Adhuhuri

بسم الله الرحمن الرحیم لا اِلهَ اِلاَّ اللهُ الْعَظيمُ الْحَليمُ لا اِلهَ اِلاَّ اللهُ رَبُّ الْعَرْشِ الْكَريمُ اَلْحَمْدُ للهِِ رَبِّ الْعالَمينَ اَللّهُمَّ اِنّي أَسْأَلُكَ مُوجِباتِ رَحْمَتِكَ وَ عَزائِمَ مَغْفِرَتِكَ وَالْغَنيمَةَ …
Jumapili, 18 Machi 2012 18:03

Dua baada ya sala ya Asubuhi

Dua baada ya sala ya Asubuhi
Mwenyezi Mungu anasema: Niombeni nitakupeni. Zifuatazo hapa ni dua za baada ya nyakati mbalimbali za sala. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atutakabalie ibada na dua zetu. Amin. ***  بسم الله الرحمن الرحیم …

Ethiopia yakosoa ukiukwaji wa haki za binadamu Afrika



Ethiopia yakosoa ukiukwaji wa haki za binadamu Afrika
Waziri Mkuu wa Ethiopia amekosoa hali ya machafuko na ukiukwaji wa haki za binadamu unaoshuhudiwa katika nchi nyingi za Afrika hususan katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Haile Mariam Desalegn ameliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba nchi za Afrika zinaendelea kusumbuliwa na machafuko na ukiukwaji wa haki za binadamu na kwamba hali hiyo inatia wasiwasi mkubwa.
Waziri Mkuu wa Ethiopia pia ametuma salamu za rambirambi kwa taifa, serikali na familia za wahanga waliouawa katika shambulizi la kigaidi kwenye jumba la madula la Westgate nchini Kenya na kusisitiza kuwa, tukio hilo linaonesha tena udharura wa jamii ya kimataifa kupambana na ugaidi na misimamo ya kufurutu mipaka. Amesema machafuko yanayotokea katika nchi za Afrika hususan katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yanatishia usalama na amani na kwamba njia pekee ya utatuzi ni kuzikutanisha pande hasimu katika meza ya mazungumzo.

Waislamu kote duniani waimarishe umoja'



'Waislamu kote duniani waimarishe umoja'
Rais Hassan Rohani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa maulamaa na shakhsia wa Kiislamu nchini Marekani ni nembo ya umoja na mshikamano wa Waislamu.
Rais Rohani aliyasema hayo jana alipokutana na maulamaa, wasomi na walinganiaji wa Kiislamu katika jamii ya Marekani na kusisitiza kuwa ulimwengu wa Kiislamu hii leo unahitajia umoja na mshikamano zaidi kuliko wakati wowote mwingine. Ameongeza kuwa maulamaa na shakhsia wa Kiislamu wa Marekani wanaweza kutoa mchango muhimu katika kukurubisha pamoja mataifa mawili ya Iran na Marekani na kutatua migogoro ya Mashariki ya Kati.
Rais Rohani amesema kuwa walinganiaji wa Kiislamu wanawajibika kutumia mbinu bora zaidi za kueneza dini na kusema kuwa, inasikitisha kwamba hii leo propaganda za kuwatisha watu kuhusu Uislamu zinafanywa kwa kiwango kikubwa.
Amesema kuwa Ulimwengu wa Kiislamu na eneo la Mashariki ya Kati linasumbuliwa na matatizo mengo baada ya uingiliaji wa nchi za kigeni, misimamo ya kufurutu mipaka, ukatili na ugaidi na akaongeza kuwa la kusikitisha zaidi ni kwamba baadhi ya ukatili huo unafanyika kwa kutumia jina la dini. 

Umoja wa Mataifa unasema kuwa wanajeshi wake wanne wa amani nchini Mali walihusika na kitendo cha kumbaka mwanamke mmoja wiki jana.


JINSI JENGO LA WESTGATE LILIVYOPATA MAJANGA


Ndio maswali yaliyoulizwa laikini hakuna majibu.

Maswali mengi kuliko majibu

wengi walifariki.

Je kulikuwa na washambuliaji wanawake?


MAHAKAMA YAKATAA RUFAA YA TAYLOR