TANGAZO

TANGAZO
WEKA TANGAZO LAKO HAPA

Alhamisi, 28 Novemba 2013

Jeshi la Syria la rejesha udhibiti wa mji wa Deir Attiyeh kwenye himaya yake

Wanajeshi wa Syria wakishangilia baada ya kufanikiwa kurejesha mji wa Deir Attiyeh


Wanajeshi wa Syria wakishangilia baada ya kufanikiwa kurejesha mji wa Deir AttiyehJeshi la Syria limedhibiti tena mji muhimu wa Deir Attiyeh leo Alhamisi , siku chache baada ya kuupoteza, ikijiweka katika nafasi nzuri katika juhudi zake za kuwasambaratisha waasi Kaskazini mwa Damascus

Jumamosi, 2 Novemba 2013

Wakuu wa Kenya wameahidi kuchukua hatua dhidi ya wabakaji

Maandamano yaliyofanywa Kenya juma hili kupinga adhabu waliyopewa wabakaji
Wakuu wa Kenya wameahidi kuchukua hatua za haraka baada ya watu wa sehemu mbalimbali za dunia kuonesha hasira juu ya ubakaji wa kikatili aliofanyiwa msichana wa miaka 16.

Marekani yakiri huenda udukuzi ukawa umevuka mipaka

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry akiri udukuzi huenda ukawa umekwenda mbali sana, haya yanajiri wakati bado mvutano unaendelea kati ya taifa hilo na mataifa ya ulaya juu ya madai ya udukuzi
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry

Kiongozi wa Taliban auawa nchini Pakistan

Shambulizi la ndege ya Marekani isiyoruka na rubani Ijumaa (01.10.2013) limemuuwa Hakimullah Mehsud, kiongozi wa Taliban nchini Pakistan. Alichukua uongozi baada ya mtangulizi wake kuuawa mwaka 2009

Jeshi la Kongo laanzisha 'awamu ya mwisho' ya kuwang'oa M23

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limeanzisha kile wanachokiita "awamu ya mwisho" kuwamaliza wapiganaji waliobakia wa M23 , baada ya kuichukua ngome ya mwisho katika hatua ya kuuvunja kabisa uasi huo.
Wanajeshi wa Kongo wakiwa katika matayarisho ya kufanya mashambulizi 'ya mwisho' dhidi ya M23.
Wanajeshi wa Kongo wakiwa katika matayarisho ya kufanya mashambulizi 'ya mwisho' dhidi ya M23.
Mkaazi mmoja wa mji wa Jomba ulio mpakani mwa Kongo na Uganda, ameliambia shirika la habari la AFP kwa njia ya simu kwamba sasa "wanajeshi wa Kongo wanaendesha operesheni zao dhidi ya waasi"kwenye eneo hilo.

Jela maisha kwa ubakaji Afrika Kusini


Johannes alikiri kumbaka Anene lakini alikanusha madai ya kumuua
Mwanamume mmoja nchini Afrika Kusini aliyepatikana na hatia ya ubakaji na mauaji ya msichana mwenye umri wa miaka 17 amepewa hukumu mbili za maisha jela na mahakama moja viungani mwa mji wa Cape Town.

Niger kuzuia maafa Jangwani Sahara


Jangwa la Sahara
Waziri wa mambo ya nje wa Niger, anasema kuwa wanawake na watoto huenda wakapigwa marufuku kusafiri nje ya nchi kupitia eneo la Kaskazini mwa nchi.

Jumatatu, 21 Oktoba 2013

Watu watatu akiwemo msichana mdogo mwenye umri wa miaka 8 wauawa

Waumini walishambuliwa wakiwa wanatoka kanisan
Watu watatu akiwemo msichana mdogo mwenye umri wa miaka 8 aliuawa wakati watu waliokuwa wamejihami wakiwa kwenye pikipiki kushambulia sherehe za ndoa nje ya kanisa la Kikopti mjini Cairo.

Boko Haram waua madereva 19 Nigeria

Mabaki ya magari ya madereva waliouawa na Boko Haram
Wanamgambo waliokuwa wamevaa nguo za kijeshi, wamewaua watu 19 katika kuzuizi cha barabarani walichokuwa wameweka kukagua magari katika jimbo la Borno.

Jumapili, 13 Oktoba 2013

Utaliana itazidisha doria Mediterranean

Wanajeshi wakisaidia katika uokozi, Lampedusa
Utaliana itazidisha doria za wanajeshi kusini mwa bahari ya Mediterranean, baada ya mamia ya wakimbizi kuzama

Upinzani wa Syria hautaki kuzungumza

George Sabra
kongozi wa kundi kubwa katika ushirikiano wa upinzani nchini Syria amesema ana hakika hatohudhuria

Hijja yaanza Makka


Malaki  ya waumini wamekusanyika Mina karibu na mji wa Saud Arabia wa Makka kuanza kutekeleza nguzo ya tano ya dini ya kiislam-Hajji.

HIVI HAWA BAKWATA WANA AKILI AU MATOPE AU NI MAKAFIRI????

Jamani waislamu tusipelekwe tu kama magari mabovu na hawa bakwata kwasababu sijui niwaweke katika kundi gani yaani hawana hata aibu wanatangaza edd jumatano haliya kua watu wana simama arafa kesho waislamu tuamke tuacheni kulala jamani.



hii ndo taarifa yao hebu isome. chanzo bakwata.

Jumamosi, 12 Oktoba 2013

Wakimbizi wengine wazama baharini


Wakimbizi kadhaa wanahofiwa kuwa wamekufa baada ya  mashua yao kuzama karibu na kisiwa cha Sicily, katika bahari ya Mediterenia nchini Italia.

Ijumaa, 11 Oktoba 2013

Pinda ampiga stop Magufuli ni mara baada ya meli, mizigo kukwama bandarini

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ametengua maamuzi yaliyofanywa na Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli ya kuongeza tozo ya asilimia tano kwa wasafirishaji wa malori na mabasi kwa uzito unaozidi.

Ajali ya moto ya ua watu kumi nchini japani

10 wafariki katika ajali ya moto ndani ya hospitali Japan

hebu skia hjii heti wabakaji nchini kenya adhabu yaokukata nyasi

Mwathiriwa alisema kuwa anawajua wabakaji
Wakenya wameghadhabishwa sana na hatua ya wanaume watatu waliombaka msichana mmoja na kutupa mwili wake kwenye choo kuamrishwa na polisi kukata nyasi kama adhabu kwao.

JK: Tunataka malaria ikome mwaka 2016


Rais Jakaya Kikwete, amesema ni dhamira ya Tanzania kuhakikisha kwamba malaria inatokomezwa kabisa hapa nchini ifikapo mwaka 2016.

AU kujadili uhusiano wake na ICC

AU inajadili swala hili baada ya ICC kupuuza ombi la kutaka kuhamisha kesi za Kenyatta na Ruto
Marais wa Afrika wanakutana wikendi hii mjini Addis Ababa nchini Ethiopia kujadili uhusiano wa bara la Afrika na mahakama ya kimataifa ya jinai ICC.