Rais wa TZ , Jakaya Kikwete
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ametangaza kuwa mgogoro baina ya Tanzania na Rwanda umemalizika.
Katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi kwa raia wa nchi hiyo Rais Kikwete amesema hatua hiyo inafuatia mazunguzo baina ya viongozi hao wawili yaliyofanyika hivi karibuni nchini Uganda