Jeshi la Rwanda limekosoa vikali vikwazo vilivyowekwa na Marekani dhidi ya nchi hiyo. Taarifa zinasema kuwa, Marekani imechukua uamuzi huo baada ya kulituhumu jeshi la Rwanda kuwa liliwasaidia waasi wa M23 wa Kongo katika kuwatumikisha watoto jeshini.
TANGAZO
WEKA TANGAZO LAKO HAPA
Ijumaa, 4 Oktoba 2013
Juhudi za uokozo zaendelea Lampedusa
Baadhi ya waliopoteza maisha yao wakitafuta kuingia Ulaya
Juhudu za uokozi zimeanza tena Kusini mwa Utaliano baada ya boti iliyokuwa imewabeba wahamiaji wa kiafrika kwenda Italia, kuzama katika kisiwa cha Lampedusa.
Muhubiri wa kiisilamu auawa Mombasa
Marehemu Aboud Rogo alidaiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la Al Shabaab
Kiongozi mmoja wa dini ya kiisilamu ameuawa kwa kupigwa risasi pamoja na watu wengine mjini Mombasa, Pwani ya Kenya.
Mazungumzo ya kitaifa Tunisia kuanza kesho
Duru ya kwanza ya mazungumzo ya moja kwa moja kati ya chama tawala cha an Nahdha nchini Tunisia na vile vya upinzani yenye lengo la kutatua mivutano ya kisiasa, itaanza hapo kesho nchini humo
13 wafariki katika ajali ya ndege Nigeria
Ndege iliyokuwa imewabeba watu 27 imeanguka baada ya kukumbwa na hitilafu ya injini, muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege mjini Lagos
Alhamisi, 3 Oktoba 2013
Mkutano wa vijana kufanyika SA
Vijana nchini Afrika Kusini wakiadhimisha siku ya vijana duniani
Kile kinachosemekana kuwa mkutano mkubwa zaidi wa vijana unatarajiwa kuanza hivi punde mjini Johannesburg nchini Afrika Kusini.
Jisajili kwenye:
Maoni
(
Atom
)