Duru ya kwanza ya mazungumzo ya moja kwa moja kati ya chama tawala cha an Nahdha nchini Tunisia na vile vya upinzani yenye lengo la kutatua mivutano ya kisiasa, itaanza hapo kesho nchini humo
Jimbo la Niedersachsen moja kati ya majimbo 16 nchini Ujerumani, limeitambua dini ya Kiislamu kuwa ni dini rasmi kwenye jimbo hilo lililoko kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
Mahakama ya kimataifa ya ICC, imetoa kibali cha kukamatwa kwa raia Mkenya ambaye anatuhumiwa kwa kujaribu kuwahonga mashahidi ili wajiondoe kwenye kesi dhidi ya Naibu Rais wa Kenya William Ruto.