TANGAZO

TANGAZO
WEKA TANGAZO LAKO HAPA

Ijumaa, 27 Septemba 2013

Tunaifanyia Tanesco mageuzi makubwa-JK


Jakaya-Kikwete-September27-2013                                                                                  Rais Jakaya Kikwete
Rais Jakaya Kikwete, amesema serikali yake inalifanyia mageuzi muhimu na marekebisho makubwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa nia ya kuharakisha jitihada za serikali kusambaza umeme kwa wananchi wengi zaidi.
Rais Kikwete aliyasema hayo jana alipokutana na kuzungumza na ujumbe wa Shirika la Misaada ya Maendeleo la Marekani la Millennium Challenge Corporation (MCC) ukiongozwa na Mtendaji Mkuu wake, Daniel Yohannes.
Yohannes alimwelezea Rais Kikwete kuhusu maendeleo ya ombi la Tanzania kuingizwa katika awamu ya pili ya misaada ya Serikali ya Marekani kupitia MCC chini ya Akaunti ya Milenia Tanzania (MCA(T)).
Nchi nyingine za Afrika ambazo maombi yao yanafikiriwa katika awamu hiyo ya pili ni Morocco, Msumbiji na Lesotho.
Tanzania ndiyo nchi iliyopokea sehemu kubwa zaidi ya msaada wa MCC duniani katika awamu ya kwanza ambapo ilipewa dola milioni 698 za Marekani.
Fedha hizo zimeingizwa katika miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara, usambazaji wa umeme vijijini, miradi ya maji na ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mafia.
Serikali ya Tanzania imeamua kuwa fedha za awamu ya pili ya MCC, zitaingizwa kupanua zaidi huduma za umeme na ujenzi wa barabara za vijijini kwa nia ya kuongeza idadi ya Watanzania wanaopata huduma za umeme na kwa nia ya kuboresha barabara za vijijini katika maeneo yanayozalisha mazao kwa wingi zaidi.
Serikali imeliweka suala la usambazaji umeme kwa Watanzania mijini na vijijini miongoni mwa maeneo yake ya kipaumbele.
Wakati anaingia madarakani mwaka 2005, ni asilimia 10 tu ya Watanzania waliokuwa wanapata umeme.
Yohannes alitaka kujua ni hatua zipi serikali inazichukua kurekebisha changamoto zinazoikabili Tanesco na hatua zinazochukuliwa kuzidi kukabiliana na matatizo ya rushwa.
Rais Kikwete alimweleza Yohannes: “Kama unavyojua, Tanesco imepitia safari ngumu na kukabiliwa na changamoto nyingi, lakini sasa tumeamua katika serikali kulifanyia mageuzi muhimu na marekebisho makubwa kwa maana ya muundo wake na pia kuangalia viwango vya malipo ambayo shirika hilo linawatoza wateja wake. Mageuzi haya katika Tanesco ni muhimu sana na yameanza kufanyika na kwa hakika serikali imedhamiria kukayamilisha mageuzi hayo kati

warioba aipiga kijembe serikali


WARI
                                                                                      Jaji Joseph Warioba

Tume ya Mabadiliko ya Katiba imelishangaa Bunge kwa ‘undumila kuwili’ wake wa kupitisha sheria mbili zinazokinzana kuhusiana na mchakato unaosimamiwa na tume hiyo.

Mwenyekiti wake, Jaji Joseph Warioba alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari, kwa lengo la kuwapa taarifa ya uendeshaji wa Mabaraza ya Katiba, ngazi ya serikali za mitaa ulivyofanyika.
Warioba alisema mikutano hiyo iliyoendeshwa na Tume ilianza Julai 12, 2013 na kumalizika Septemba 2, mwaka huu.
Alisema wakati Sheria Mama iliyoiunda Tume ya yake mwaka 2011 inatamka kwamba Tume iendelee kuwapo katika mchakato wote, hadi pale kura ya maoni ya kupitisha au kukataa Katiba mpya itakapofanyika.
Hata hivyo, alisema Muswada wa Sheria ya  Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2013 uliopitishwa katika mkutano wa Bunge wa 12, umekataa hilo.
Muswada huo uliungwa mkono na kupitishwa na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) na Augustine Mrema (TLP), lakini wabunge wa upinzani wa Chadema,CUF na NCCR-Mageuzi waliupinga na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge.
Jaji Wariona alisema marekebisho yaliyofanywa katika kikao cha 12 yanakinzana na Sheria mama kwa sababu, Muswada wa sasa unataja muda wa Tume kumalizika pale itakapowasilisha Rasimu ya Katiba, katika Bunge Maalum la Katiba.
“Tunajua kazi ya kutunga sheria si ya kwetu, ni ya wengine, na hata sheria inayotuongoza katika utendaji kazi wetu, tumeikuta ikiwa imeshatungwa tayari na wahusika, na hakika sisi tunafanya kazi kulingana na sheria iliyo mbele yetu,” alisema.
Jaji Warioba alisema hata hivyo kwamba, wakati Muswada wa Marekebisho unahitimisha ukomo wa Tume baada ya kuwasilisha Rasimu katika Bunge Maalumu la Katiba, Sheria mama inawataka waendelee mpaka kwenye hatua ya kura ya maoni.
Alisema Sheria mama inaitaka Tume iendelee mpaka kwenye hatua hiyo, ili pamoja na mambo mengine iweze kutoa elimu kwa wananchi.
“Sasa utafanya jukumu hilo kwa kutumia mamlaka ipi, wakati tayari shughuli zako zimefikia ukomo baada ya kuwasilisha Rasimu kwenye Bunge Maalum la Katiba?” alihoji Jaji Warioba.
KUJIUZULU WAJUMBE WA TUMEJaji Warioba alizungumzia pia taarifa zilizoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari za baadhi ya wajumbe wa Tume kutishia kujiuzulu kama ishara ya kupinga Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba uliopitishwa na Bunge hivi karibuni.
“Siyo kweli kuwa wanataka kujiuzulu. Kilichotokea ni kuwa baada ya safari ya kuzunguka karibu nchi nzima, na kukutana na changamoto nyingi ambazo ziliwachosha, zikiwemo za matamshi ya Kuwadhalilisha,” alisema.
Alisema baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa walitoa matamshi yaliyolenga kuwadhalilisha wajumbe wa Tume, na kuishusha thamani kazi iliyofanywa na Tume ya kuandika Rasimu ya Katiba.
“Aidha baadhi ya viongozi wa siasa pia walitoa matamshi yaliyowalenga wajumbe wa Tume, na kuwafanya baadhi ya wajumbe wa Mabaraza, kuwajadili wajumbe wa Tume, badala ya Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume,” alisema.
Hata hivyo, Jaji Warioba hakutoa maelezo zaidi kuhusiana na matamshi yaliyotolewa dhidi ya wajumbe wa Tume yake.
Alisema ni katika vikao vya kupitia safari hizo za wajumbe na changamoto walizokumbana nazo pamoja na uchovu waliokuwa nao kutokana na changamoto hizo, ndipo baadhi ya wajumbe walipoonekana kusema bwana basi, lakini hawakusema wanataka kujiuzulu.
Alisema Katiba inayotafutwa ni ile itakayoleta umoja wa Watanzania wote na ambayo itakuwa chachu ya maendeleo ya nchi kwa vizazi vijavyo.
“Hatutafuti katiba ya kundi moja au ya chama kimoja, au katiba itakayotokana na mapambano, kwa hiyo ni muhimu kwa viongozi wa kisiasa, wakaona busara ya kukaa pamoja na kuondoa tofauti zao,” alisema.
Jaji Warioba alisema, katiba yenye kuleta umoja haitapatikana kwa njia ya maandamano au malumbano ya kwenye majukwaa, na badala yake itapatikana kwa njia ya kuzimaliza tofauti walizonazo, kwa njia ya mazungumzo.
IDADI YA MIKUTANOIli kuendesha mikutano ya Mabaraza ya Katiba kwa ufanisi, Jaji Warioba alisema Tume ilijigawa katika makundi 14, kila kundi likiwa na wajumbe wawili au watatu.
Alisema makundi hayo yalizunguka nchi nzima na kufanya mikutano 179, iliyohudhuriwa na wajumbe 19,337, ambayo ilifanyika katika kila Halmashauri ya wilaya, Halmashauri ya Manispaa na jiji, huku mkutano mmoja ukidumu kwa wastani ya siku tatu.
Alisema jumla ya mikutano 166 ilifanyika Tanzania Bara na 13 ilifanyika Tanzania Zanzibar.
CHANGAMOTOAlisema baadhi ya changamoto zilizojitokeza ni za baadhi ya vyama vya siasa kuingilia uhuru wa wajumbe katika kutoa maoni yao kuhusu rasimu ya katiba.
Aidha, alizitaja zingine kuwa, ni kwenye baadhi ya maeneo, wajumbe wa Mabaraza ya Katiba walifundishwa nini cha kusema juu ya Rasimu ya Katiba, na baadhi ya vyama vya siasa kuendesha mikutano ya hadhara na ya ndani ya wanachama wao, sambamba na mikutano ya mabaraza.
KINACHOENDELEAJaji warioba alisema, kinachofanyika kwa sasa ni uchambuzi wa maoni yaliyotolewa na Mabaraza ya Katiba, kwa kufuata mwongozo ambao Tume imejiwekea na uchambuzi unafanywa kwa kuzingatia uzito wa hoja, zilizotolewa na wananchi katika maeneo tofauti ya Rasimu ya Katiba.
Alisema baada ya uchambuzi, Tume itaandaa Ripoti itakayojumuisha Rasimu ya Katiba iliyoboreshwa kutokana na maoni ya Mabaraza ya Katiba na kuiwasilisha kwa Rais wa Tanzania na wa Zanzibar, kama Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inavyolelekeza.
“Mipango ya Tume ni kukamilisha kazi hii ndani ya muda uliowekwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83,” alisema.
MJUMBE AITUMUMU CCMWakati Jaji Warioba akisema hayo, Mjumbe wa Tume hiyo, Dk. Sengondo Mvungi, amesema Chama Cha Mapinduzi)  kinaandaa rasimu yake ya Katiba Mpya, ili kiiwasilishe kinyemela kupitia kwa wabunge wake kwenye Bunge la Katiba litakalofanyika Novemba mwaka huu.
Alisema kuwa rasimu hiyo ni tofauti na  iliyotolewa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kwamba kutokana na hali hiyo, yuko  tayari kujiuzulu ujumbe katika tume hiyo ili kuepukana na aibu kutokana na CCM na serikali kuamua kuvuruga kwa makusudi mchakato wa kupata katiba mpya inayokidhi matakwa ya wananchi wote.
Aliliambia NIPASHE jana kuwa ni aibu kubwa kwa CCM kuamua kuandaa rasmu yake huku kikijua chombo kilichopewa mamlaka hayo ni Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kushiriki maadhimisho ya miaka 18 ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na kusema kuwa anazo taarifa za uhakika kwamba mpango huo wa CCM umeandaliwa na makada wa chama na umeishakamilika hivi sasa.
Dk. Mvungi alisema CCM kimemaliza kuandaa rasimu hiyo na kwamba kitaiwasilisha katika Bunge la Katiba na wabunge wake wamejipanga kuitetea mpaka ipite.
Alisema hali ni mbaya kwa tume kwa kuwa imeingiliwa na CCM na serikali yake na kwamba mambo yakiendelea hivyo, wake watajiondoa.
Amesema kwa upande wake yupo tayari kujiuzulu na kukaa pembeni badala ya kuendelea kupata aibu huku Watanzania wakimtazama.
“Mimi nipo tayari, nasubiri wajumbe wenzangu, wakisema kujiondoe hata sasa mimi nipo tayari kufanya hivyo kwa kuwa sikuingia kule kutafuta fedha, bali kuwawakilisha wananchi,” alisema Dk. Mvungi
“Aina ya sasa iliyotumika kuandika Katiba hii imewachanganya CCM na serikali na sasa wameamua kuvuruga mchakato kwa makusudi,” aliongeza Dk. Mvungi.
Alitaja mambo matatu ambayo yanaichangana CCM na serikali ni pamoja na rasimu hiyo kutamka suala la kuwapo serikali tatu, mbunge kuwekewa ukomo wa vipindi  vitatu vya miaka 15 na wabunge kutokuwa mawaziri.
KAULI YA MANGULAAkizungumzia tuhuma hizo, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula, alikanusha na kusema siyo za kweli.
Mangula baada ya kupokea simu jana jioni alisema alikuwa kwenye kikao Bagamoyo mkoani Pwani.
MAALIM SEIF: JK USISAINIMakamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hmad, amemuomba Rais Jakaya Kikwete kutousaini muswada huo badala yake ufanyiwe kwanza marekebisho.
Maalim Seif alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na Wazanzibari wanaoishi Tanzania Bara na kufafanua kuwa Wazanzibar hawakushirikishwa katika kutoa maoni.
Aidha, alisema Rasimu ya Katiba mpya inapaswa kutamka Serikali ya Tanganyika badala ya Tanzania Bara katika mfumo wa Muungano wa serikali tatu za  Zanzibar, Tanganyika na Shirikisho.
Imeandikwa na Raphael Kibiriti, Richard Makore na Muhibu Said.

mbowe nae anena mazito khus katiba



Mbowe: Katiba Mpya inahitaji hekima, busara

“Hebu angalieni sasa hivi kuna ugomvi wa dini, wananchi na Serikali hususan katika maeneo yaliyo na madini, vyombo vya usalama na raia na mengine mengi. Je hii ndiyo Tanzania yenye amani na mshikamano aliyoiacha Hayati Baba wa Taifa?” Mbowe 

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema, kukusanya maoni ya wananchi kwa ajili ya kupata Katiba Mpya siyo kazi rahisi, ni kazi inayohitaji nia ya dhati ya taifa zima, kwa kuwa katiba ni mali ya wananchi na rasilimali za taifa.Mbowe alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wa hadhara wa kukujadili Rasimu ya Maoni ya Katiba, uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo wilayani Musoma Mkoa wa Mara hivi karibuni.
Alisema kwa kutambua umuhimu wa kazi hiyo, Chadema wameamua kuzunguka nchi nzima kwa lengo la kutoa elimu ya Katiba kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na kutoa ufafanuzi wa maana ya Katiba na kujibu hoja za wananchi hao.
Alisema kuwa Tanzania ambayo ilikuwa ikisifika kama nchi ya amani na mshikamano kwa miaka mingi, sasa inaelekea kubomoka na hali hiyo inatokana na katiba mbovu isiyokuwa na mipaka ya madaraka ambayo sasa tumeamua kuifanyia mabadiliko.
“Hebu angalieni sasa hivi kuna ugomvi wa dini, wananchi na Serikali hususan katika maeneo yaliyo na madini, vyombo vya usalama na raia na mengine mengi. Je hii ndiyo Tanzania yenye amani na mshikamano aliyoiacha Hayati Baba wa Taifa?” alihoji Mbowe.
Alisema katika kuzungumzia Katiba hakuna vyama vya siasa, polisi wala mtu wa kada nyingine yoyote. Katiba ni mali ya Watanzania wote, hivyo kila mmoja ana wajibu wa kutoa maoni yake juu ya mambo anayoamini kuwa yatalisaidia taifa kama yataingizwa kwenye katiba.
Awali akihutubia katika mkutano huo,Mmbunge wa Ubungo John Mnyika, alisema kuwa maadili ya uongozi na utawala bora, vinatikiswa kama siyo kuyumbishwa. Aliwataka wananchi kuhakikisha misingi ya taifa inarekebika kupitia marekebisho ya katiba mpya.
Mnyika alisema kuwa katika kupitisha maoni ya katiba, wanataka haki, uwazi na usawa katika masuala ya madini na rasilimali za nchi ambazo kimsingi zinapaswa kutajwa kwenye katiba. Tunataka Katiba pia impunguzie rais madaraka, alisema.
Alisema gharama za maisha ya wananchi zinazidi kupanda kila kukicha kutokana na rais kuwa na mlimbikano wa madaraka, hivyo kufanya maamuzi bila kutambua kuwa wananchi walio na kima cha chini ndio wanaoumia.
Aidha alisema kuwa anashangazwa na serikali ya CCM inavyokataa mfumo wa serikali tatu kwa madai kuwa,serikali tatu ni gharama kubwa sana kuendesha huku wakisahau baraza kubwa la mawaziri lisilo na meno.
Chadema imekuwa ikifanya mikutano ya hadharani nchini kuzungumzia mchakato wa katiba. Wamekuwa wakitoa elimu na kuwaeleza wananchi umuhimu wa kazi hiyo kwa taifa.

Nyie ni watu wabaya

 Mtoto wa miaka 4 awaambia magaidi



  • Magaidi walionekana kuumizwa na kauli za mtoto aliyewaambia kuwa wao ni watu wabaya, wakamwomba msamaha na kumpa chokleti.


Mtoto wa miaka minne ambaye ni raia wa Uingereza, Elliott Prior ameonyesha ushujaa wa hali ya juu baada ya kuweza kuwatolea maneno makali na ya kugusa magaidi waliovamia jengo la maduka la Westgate.Baada ya maneno hayo, baadhi ya taarifa zilizochapishwa kwenye vyombo mbalimbali vya kimataifa, vinasema magaidi hao waliomba mtoto huyo awasamehe kwa maelezo kuwa wao siyo watu wabaya.
Inaelezwa kuwa, kitendo cha mtoto huyo kilikuwa cha kishujaa kwani aliweza kuwaeleza magaidi hao maneno hayo, bila kuogopa silaha nzito walizokuwa wameshika mkononi huku baadhi ya watu wakiwa wameshauuawa.
Mtandao wa Daily Mail unasema mtoto huyo alimwambia mmoja wa magaini hao kuwa ‘Nyie ni watu wabaya sana’.
Mtandao huo unasema mtoto huyo aliyasema maneno hayo kama njia ya kumkinga mama yake Amber, aliyekuwa amepigwa risasi mguuni pamoja na dada yake Amelie, mwenye umri wa miaka sita ambaye walikuwa wote ndani ya duka hilo.
Katika kile kilichotafsiriwa kuwa ni kuumizwa na maneno hayo, magaidi hao walimpa Elliott pamoja na dada yake mifuko miwili miwili ya chokleti na kuwaomba msamaha.
Taarifa hizo zinasema kuwa,  gaidi huyo alisema “Samahani nisamehe, sisi siyo watu wabaya”.
Mama huyo anasema kuwa, kabla ya kukamatwa na magaidi hao, yeye na watoto wake walikuwa wamejificha kwenye jokofu la kuhifadhi nyama lililopo ndani ya duka la Nakumatt kwa zaidi ya saa moja na  nusu.
Anasema kuwa, baada ya kukamatwa na magaidi hayo, walimpiga risasi ya paja.
Mjomba wa watoto hao aliliambia gazeti la The Sun la Uingereza kuwa  “Walikuwa na bahati kuweza kutoka kwenye mikono ya hao magaidi. Hao magaidi walisema kuwa, kama kuna mtoto yeyote aliye hai ndani ya jengo hilo wanaweza kuondoka.
‘Mama yao alisimama na kusema ‘ndio’ , binamu yangu aliweza kupata ujasiri wa kusimama na kuwaambia kuwa, nyie ni watu wabaya sana’.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, baada ya magaidi hao kujua kuwa mama huyo na watoto wake hawakuwa kati ya watu waliowalenga, hawakuwaua.


Abdul Haji:Mkenya aliyekuwa tayari kuuawa


Abdul Haji akimwokoa mtoto asiuawe na magaidi. Picha ya maktaba 


Wakati vyombo vya usalama vya Kenya vikitangaza kulidhibiti jengo lote la Westgate lililovamiwa na magaidi wanaodaiwa kuwa wa kundi la Al-Shabaab, baadhi ya watu waliojitoa muhanga na kufanikiwa kuokoa maisha ya wengine, wanaendelea kuibuka.Hivi karibuni gazeti hili lilichapisha habari juu ya askari wa Kikosi Maalumu cha Anga (SAS) cha Uingereza, aliyeweza kuokoa zaidi ya watu 100 ndani ya jengo hilo.
Hivi karibu, baadhi ya vyombo vya habari vya Kenya vimemnukuu pia  Abdul Haji (38) ambaye ni raia wa kawaida aliyeweza kufika ndani ya jingo hilo na kuokoa watu waliokuwa wametekwa na wanamgambo hao wanaodaiwa kuwa wa Al Shabaab.
Gazeti la Daily Nation, limemnukuu kijana huyo akisema alipata ujumbe mfupi wa simu ya mkononi (SMS) kutoka kwa kaka yake ukisomeka kuwa “Nimekwamba Westgate, nadhani kuna magaidi wamevamia hapa, niombee”.
Kijana huyo ambaye asili yake ni Msomali, alisema alipata sana hofu kutokana na ujumbe huo wa kaka yake kwani ilikuwa ni wiki mbili tu tangu televisheni moja ya nchi hiyo kumtaja kaka yake huyo kama mmoja wa watu anaowasaidia magaidi hao wa Al Shabaab.
Kijana huyo ambaye ni mtoto wa Seneta, Yusuf Haji alisema hali hiyo ilimpa wasiwasi zaidi kwani tayari walishaanza kupata vitisho kutoka kwa baadhi ya watu wakiamini kuwa kweli familia yake wanawasaidia Al Shabaab.
Anasema baada ya ujumbe huo alikimbia mara moja na kwenda katika jengo hilo la Westgate, na muda mfupi tu tangu magaidi hao kuingia ndani ya jengo hilo na kuanza kuwafetulia watu risasi alikuwa ameshawasili eneo hilo.
Haji ambaye ni mfanyabishara na baba wa watoto wane wa kike, alisema aliamini kuwa magaidi hao walikuja kumfuata kaka yake na baadaye familia nzima hivyo aliamua kujitoa muhanga ili kumuokoa kaka yake na familia yake yote.
Mtoto huyo ambaye baba yake ni Seneta wa Garissa na aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ulinzi wan chi hiyo, alisema aliingia kwenye jengo hilo akiwa na bastola ambayo anaimiliki kwa kufuata sheria zote za Kenya.
Anasema kuwa, alipofika ndani ya jengo hilo aliona watu wengi wakiwa wameuwawa wakiwa wamelala chini na wengine wakiwa bado wapo hai huku milio ya risasi ikiendelea kulia kila kona.
Aliungana na watu wengine kama 10 waliokuwa ndani ya jengo hilo ambao pia walikuwa na silaha ili waone namna  ya kusaidia baadhi ya watu.
 “Nimewahi kuona miili ya watu waliokufa lakini sijawahi kuiona mingi kama ile ikiwamo ya watoto na kinamama wasiojiweza,” anasema Haji

Warioba: nae izungumzia kuhus katba

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu, Joseph Warioba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Makamu wake, Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani. Picha na Fidelis Felix 

*******************************************************************************************************************************************************************

Dar es Salaam. Wakati wananchi wa kada mbalimbali wakishinikiza Rais Jakaya Kikwete kutokusaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba 2013, kwa maelezo kuwa una kasoro, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba naye amesema sheria ina upungufu.

Warioba alisema jana kwamba ni jambo la kushangaza sheria hiyo kueleza kuwa tume hiyo itavunjwa baada ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalumu la Katiba, wakati huohuo ikieleza kuwa itahusika tena kusimamia utoaji wa elimu ya kura ya maoni.

Kauli hiyo ya Warioba imekuja wakati vyama vya NCCR Mageuzi, Chadema na CUF, vikifanya mikutano nchi nzima kuwashawishi wananchi kupinga kile wanachokiita hujuma dhidi ya upatikanaji wa Katiba Mpya.
Muswada huo ulipitishwa na wabunge wa CCM baada ya wale wa upinzani kutoka nje baada ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe kuamuriwa na Naibu Spika, Job Ndugai kutoka nje kutokana na kukaidi kwake amri ya kukaa chini alipokuwa akitaka kutoa hoja kabla ya mjadala wake kuanza.
Muswada huo unapingwa kwa kuwa Rais amepewa mamlaka ya kuteua wajumbe 166, ambao si wabunge wala wawakilishi na Zanzibar kutokushirikishwa kikamilifu kwenye maandalizi ya muswada huo.
Alisema baada ya kuipata sheria hiyo: “Tulijiuliza maswali kwa sababu miswada huwa inapelekwa bungeni na Serikali ikiwemo ya Katiba. Anayeipeleka kama ni waziri ndiye anayetoa ufafanuzi pale inapohitajika.”

Sheria hiyo ambayo Warioba amesema ina upungufu, muswada wa marekebisho yake ulijadiliwa na kupitishwa wa wabunge Septemba 6, mwaka huu katika Mkutano wa 12 wa Bunge Mjini Dodoma, ikiwa ni baada ya kubadilishwa kwa baadhi ya vifungu na hivi sasa Rais Kikwete anasubiriwa kuusaini ili iwe sheria kamili. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Jaji Warioba alisema: “Mwisho wa kazi ya tume ni baada ya kukabidhi rasimu, hilo ni tatizo. Maana tume itakuwa imeshavunjwa, sasa itafanyaje kazi ya kutoa elimu kwenye kura ya maoni?”

Jaji Warioba pamoja na kukiri upungufu huo, alisema kurekebisha au kutokurekebisha kasoro hizo si jukumu la tume hiyo.

“Tunawaomba watafakari, waone jinsi gani tume ambayo imekwishavunjwa itakuja kutoa elimu wakati wa kura ya maoni, sheria ina ‘contradiction’ (ina mkanganyiko),” alisema.

Hata hivyo, Warioba alisema pamoja na kasoro hizo Tume hiyo inafanya kazi yake kwa kufuata sheria hiyo huku akisisitiza, “Wanaotunga sheria ni wengine siyo sisi, tulipoteuliwa tulikuta sheria na kuanza kazi kwa kuifuata. Imefanyiwa marekebisho sisi tunafuata.”

Alisema waliofanya mabadiliko ya sheria hiyo wana haki ya kufanya hivyo na kwamba Tume ya Mabadiliko ya Katiba haiwezi kuzuia kutokufanyika kwa mabadiliko hayo, kwani yapo baadhi yanaihusu.

Alisema kulingana na sheria, tume yake ndiyo inayotakiwa kutoa ufafanuzi katika Bunge la Katiba, kama ambavyo Waziri hutoa maelezo anapowasilisha muswada bungeni.

Katiba mpya Tanzani bado majanga kwa vyama pinzani

Katiba mpya Tanzani bado majanga kwa vyama pinzani

Prof Ibrahimu Lipumba

Chama cha Wananchi (CUF) kimesema kinaungana na Watanzania walioonyesha shaka juu ya mchakato wa kupata Katiba mpya kwani hakioni nia njema na utayari wa Tume kuwa na Katiba inayotokana na maoni ya wananchi.

Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Irahim Lipumba, alisema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maazimio ya kikao cha baraza kuu la chama hicho kitaifa.


Alitaka  Rasimu ya Katiba inayoandaliwa iwekwe hadharani kwa wakati ili wananchi waweze kutoa maoni yao kabla haijapelekwa katika Bunge la Katiba na kupigiwa kuwa na wananchi.

Alisema Cuf hakitakuwa tayari kuiunga mkono Katiba ambayo haitakuwa na misingi imara ya kidemokrasia na isiyotokana na maoni ya Watanzania na kitakuwa tayari kuwahamasisha kuikataa katiba hiyo.

Profesa Lipumba ameitaka tume ya kuratibu ukusanyaji wa maoni kuweka mpango wa kuyafikia makundi yenye mahitaji maalumu ikiwa ni wanawake, walemavu, vijana na asasi za kiraia zinazoshughulika na malezi ya watoto ili yaweze kutoa maoni yao.

Alisema pamoja na mchakato wa uandikaji wa katiba kupangiwa miezi 18 muda huo  hautoshi  kwani kuna chaguzi mbalimbali ambazo zinatarajiwa kufanyika mwakani hivyo hakuna sababu za msingi za kuharakisha zoezi hilo na kupata katiba mbovu isiyokidhi matakwa ya wananchi na badala yake kupata katiba ya matakwa ya kikundi kidogo cha watu wenye dhamana.

hata hivyo prfesa lipumba amewataka wananchi wasipelekwe pelekwe tu kama gari bovu na wala wasifuate upepo kama bendera amesema nilazima wananchi washirikishwe kikamailifu ili ipatikane katiba bora na yenye tija, ametaka na watu wa wazenjibari nawao washirikishwe na akamalizia kwa kusema kua kila mtanzania ana haki ya kutoa ushauri juu ya mchakato wa katiba mpya.