TANGAZO

TANGAZO
WEKA TANGAZO LAKO HAPA

Alhamisi, 28 Novemba 2013

Jeshi la Syria la rejesha udhibiti wa mji wa Deir Attiyeh kwenye himaya yake

Wanajeshi wa Syria wakishangilia baada ya kufanikiwa kurejesha mji wa Deir Attiyeh


Wanajeshi wa Syria wakishangilia baada ya kufanikiwa kurejesha mji wa Deir AttiyehJeshi la Syria limedhibiti tena mji muhimu wa Deir Attiyeh leo Alhamisi , siku chache baada ya kuupoteza, ikijiweka katika nafasi nzuri katika juhudi zake za kuwasambaratisha waasi Kaskazini mwa Damascus

Jumamosi, 2 Novemba 2013

Wakuu wa Kenya wameahidi kuchukua hatua dhidi ya wabakaji

Maandamano yaliyofanywa Kenya juma hili kupinga adhabu waliyopewa wabakaji
Wakuu wa Kenya wameahidi kuchukua hatua za haraka baada ya watu wa sehemu mbalimbali za dunia kuonesha hasira juu ya ubakaji wa kikatili aliofanyiwa msichana wa miaka 16.

Marekani yakiri huenda udukuzi ukawa umevuka mipaka

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry akiri udukuzi huenda ukawa umekwenda mbali sana, haya yanajiri wakati bado mvutano unaendelea kati ya taifa hilo na mataifa ya ulaya juu ya madai ya udukuzi
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry

Kiongozi wa Taliban auawa nchini Pakistan

Shambulizi la ndege ya Marekani isiyoruka na rubani Ijumaa (01.10.2013) limemuuwa Hakimullah Mehsud, kiongozi wa Taliban nchini Pakistan. Alichukua uongozi baada ya mtangulizi wake kuuawa mwaka 2009

Jeshi la Kongo laanzisha 'awamu ya mwisho' ya kuwang'oa M23

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limeanzisha kile wanachokiita "awamu ya mwisho" kuwamaliza wapiganaji waliobakia wa M23 , baada ya kuichukua ngome ya mwisho katika hatua ya kuuvunja kabisa uasi huo.
Wanajeshi wa Kongo wakiwa katika matayarisho ya kufanya mashambulizi 'ya mwisho' dhidi ya M23.
Wanajeshi wa Kongo wakiwa katika matayarisho ya kufanya mashambulizi 'ya mwisho' dhidi ya M23.
Mkaazi mmoja wa mji wa Jomba ulio mpakani mwa Kongo na Uganda, ameliambia shirika la habari la AFP kwa njia ya simu kwamba sasa "wanajeshi wa Kongo wanaendesha operesheni zao dhidi ya waasi"kwenye eneo hilo.

Jela maisha kwa ubakaji Afrika Kusini


Johannes alikiri kumbaka Anene lakini alikanusha madai ya kumuua
Mwanamume mmoja nchini Afrika Kusini aliyepatikana na hatia ya ubakaji na mauaji ya msichana mwenye umri wa miaka 17 amepewa hukumu mbili za maisha jela na mahakama moja viungani mwa mji wa Cape Town.