Maafisa wa utawala nchini Nigeria wanasema kuwa hapakuwa na ulinzi katika chuo cha mafunzo ya kilimo nchini Nigeria ambako hadi wanafunzi 50 waliuawa Jumapili.
Kamati ya bunge inayohusika na ulinzi na uhusiano na mataifa ya kigeni imependekeza kufungwa kwa kambi za wakimbizi nchini Kenya, ikisema zinatishia usalama wa nchi.
Msemaji wa Jumuiya ya Kiislamu ya Colombia amesema kuwa, walimwengu wanapaswa kuzingatia hatari ya silaha za atomiki za utawala wa Kizayuni wa Israel. Rashid Caravali amesisitiza kwamba, umewadia wakati sasa kwa nchi za Mashariki ya Kati na nchi nyingine ulimwenguni kuipa uzito hatari ya silaha za nyuklia za utawala haramu wa Israel hasa kwa kuzingatia kwamba, utawala huo mara kadhaa wa kadhaa umeonesha wazi na bila kificho uadui wake kwa nchi za eneo. Msemaji wa Jumuiya ya Kiislamu ya Colombia ameongeza kuwa, Israel sio tu kwamba, inamiliki silaha za kemikali bali inazo pia silaha za nyuklia ambazo ni tishio kubwa kwa usalama wa dunia hususan eneo la Mashariki ya Kati. Rashid Caravali amesema, jamii ya kimataifa inapaswa kuushinikiza utawala huo ghasibu ili uangamize silaha zake zote za atomiki na kwa muktadha huo eneo la Mashariki ya Kati litashuhudia amani na utulivu.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria amesema kuwa, serikali ya Damascus haitokubali mpango wowote wa amani wa kukabidhi madaraka kwa ajili ya nchi hiyo ambao hautomshirikisha Rais Bashar al Assad.
wwwbinhafidhi Umoja wa Falme za Kiarabu, Imarati umemwita nyumbani balozi wake wa nchini Tunisia kulalamikia wito wa Rais wa nchi hiyo Moncef Marzouki kutaka Muhammad Morsi, rais wa Misri aliyeondolewa madarakani na jeshi na kuwekwa kizuizini hadi sasa, aachiliwe huru. Akihutubia mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa juzi Alkhamisi, Rais wa Tunisia aliwataka watawala wapya wa Misri wanaoungwa mkono na baadhi ya nchi za Kiarabu ikiwemo Imarati wamwachie huru Rais halali wa nchi hiyo Muhammad Morsi aliyeondolewa madarakani Julai 3 katika mapinduzi yaliyoongozwa na jeshi. Gazeti la Al- Khaleej linaloakisi misimamo ya serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu limekosoa hotuba ya Rais wa Tunisia kwa kuishambulia serikali ya mpito ya Misri na kusisitiza kuwa kinachotakiwa kufanywa ni kuiunga mkono serikali ya Cairo ambayo imekuja madarakani kwa matakwa ya wananchi. Baada ya jeshi kumuondoa madarakani Morsi, Umoja wa Falme za Kiarabu, Saudi Arabia na Kuwait ziliunga mkono mapinduzi hayo na kuahidi kuipatia kwa pamoja Misri msaada wa dola milioni 12 kusaidia uchumi wake uliozorota…/