Wakuu wa Kenya wameahidi kuchukua hatua za haraka baada ya watu wa sehemu mbalimbali za dunia kuonesha hasira juu ya ubakaji wa kikatili aliofanyiwa msichana wa miaka 16.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry akiri udukuzi huenda ukawa umekwenda mbali sana, haya yanajiri wakati bado mvutano unaendelea kati ya taifa hilo na mataifa ya ulaya juu ya madai ya udukuzi
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry
Shambulizi la ndege ya Marekani isiyoruka na rubani Ijumaa (01.10.2013) limemuuwa Hakimullah Mehsud, kiongozi wa Taliban nchini Pakistan. Alichukua uongozi baada ya mtangulizi wake kuuawa mwaka 2009
Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limeanzisha kile wanachokiita "awamu ya mwisho" kuwamaliza wapiganaji waliobakia wa M23 , baada ya kuichukua ngome ya mwisho katika hatua ya kuuvunja kabisa uasi huo.
Wanajeshi wa Kongo wakiwa katika matayarisho ya kufanya mashambulizi 'ya mwisho' dhidi ya M23.
Mkaazi mmoja wa mji wa Jomba ulio mpakani mwa Kongo na Uganda, ameliambia shirika la habari la AFP kwa njia ya simu kwamba sasa "wanajeshi wa Kongo wanaendesha operesheni zao dhidi ya waasi"kwenye eneo hilo.
Johannes alikiri kumbaka Anene lakini alikanusha madai ya kumuua
Mwanamume mmoja nchini Afrika Kusini aliyepatikana na hatia ya ubakaji na mauaji ya msichana mwenye umri wa miaka 17 amepewa hukumu mbili za maisha jela na mahakama moja viungani mwa mji wa Cape Town.
Watu watatu akiwemo msichana mdogo mwenye umri wa miaka 8 aliuawa wakati watu waliokuwa wamejihami wakiwa kwenye pikipiki kushambulia sherehe za ndoa nje ya kanisa la Kikopti mjini Cairo.