
Rais Banda amewafuta kazi mawaziri wake wote kutokana na ufisadi
Rais wa Malawi, Joyce Banda amelifuta kazi baraza lake la mawaziri kutokana na kuongezeka kwa visa vya ufisadi serikalini.
Maafisa wa serikali wamekuwa wakipatikana na pesa zikiwa zimefichwa chini ya vitanda vyao na kwenye magari yao, kwa mujibu wa mwandishi wa BBC Raphael Tenthani.




