TANGAZO

TANGAZO
WEKA TANGAZO LAKO HAPA

Ijumaa, 4 Oktoba 2013

Muhubiri wa kiisilamu auawa Mombasa

Marehemu Aboud Rogo alidaiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la Al Shabaab
Kiongozi mmoja wa dini ya kiisilamu ameuawa kwa kupigwa risasi pamoja na watu wengine mjini Mombasa, Pwani ya Kenya.

Mazungumzo ya kitaifa Tunisia kuanza kesho

Tunisia

Duru ya kwanza ya mazungumzo ya moja kwa moja kati ya chama tawala cha an Nahdha nchini Tunisia na vile vya upinzani yenye lengo la kutatua mivutano ya kisiasa, itaanza hapo kesho nchini humo

jimbo jingine Ujerumani lautambua rasmi Uislamu

Ujerumani








Jimbo la Niedersachsen moja kati ya majimbo 16 nchini Ujerumani, limeitambua dini ya Kiislamu kuwa ni dini rasmi kwenye jimbo hilo lililoko kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

13 wafariki katika ajali ya ndege Nigeria



Ndege
Ndege iliyokuwa imewabeba watu 27 imeanguka baada ya kukumbwa na hitilafu ya injini, muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege mjini Lagos

Alhamisi, 3 Oktoba 2013

Mkutano wa vijana kufanyika SA

Vijana nchini Afrika Kusini wakiadhimisha siku ya vijana duniani
Kile kinachosemekana kuwa mkutano mkubwa zaidi wa vijana unatarajiwa kuanza hivi punde mjini Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Uchunguzi wa DNA kwa viungo vya miili Kenya

Chumba cha kuhifadhia maiti cha baraza la jiji la Nairobi
Jamaa ya baadhi ya wakenya waliopotea kufuatia shambulizi la kigaidi la Westgate wamejitokeza kufanyiwa uchunguzi wa chembechembe za DNA.
Polisi walitoa ombi hilo baada ya kupata viungo vya mwili katika jengo hilo

Kibali cha ICC kumkamata mwandishi Kenya


Walter Barasa

Mahakama ya kimataifa ya ICC, imetoa kibali cha kukamatwa kwa raia Mkenya ambaye anatuhumiwa kwa kujaribu kuwahonga mashahidi ili wajiondoe kwenye kesi dhidi ya Naibu Rais wa Kenya William Ruto.