Ripoti mpya iliyotolewa na Umoja wa Mataifa imesema kuwa idadi ya watu wanaokimbia vita na machafuko katika Jamhuri ya Kidemokrasia ay Congo imeongezeka na kuwa zaidi ya laki tatu na nusu katika miezi ya hivi karibuni.
Kwa akali watu 10 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa baada ya kujiri mapigano makali kati ya wapiganaji wa kundi la Alliance of Patriots for a Free and Sovereign Congo APCLS na wanamgambo wa kundi la Sheka katika eneo la Kalembe mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Maafisa wa utawala nchini Nigeria wanasema kuwa hapakuwa na ulinzi katika chuo cha mafunzo ya kilimo nchini Nigeria ambako hadi wanafunzi 50 waliuawa Jumapili.
Kamati ya bunge inayohusika na ulinzi na uhusiano na mataifa ya kigeni imependekeza kufungwa kwa kambi za wakimbizi nchini Kenya, ikisema zinatishia usalama wa nchi.