TANGAZO

TANGAZO
WEKA TANGAZO LAKO HAPA

Jumapili, 29 Septemba 2013

‘Hatari ya silaha za nyuklia za Israel izingatiwe’


‘Hatari ya silaha za nyuklia za Israel izingatiwe’


Msemaji wa Jumuiya ya Kiislamu ya Colombia amesema kuwa, walimwengu wanapaswa kuzingatia hatari ya silaha za atomiki za utawala wa Kizayuni wa Israel. Rashid Caravali amesisitiza kwamba, umewadia wakati sasa kwa nchi za Mashariki ya Kati na nchi nyingine ulimwenguni kuipa uzito hatari ya silaha za nyuklia za utawala haramu wa Israel hasa kwa kuzingatia kwamba, utawala huo mara kadhaa wa kadhaa umeonesha wazi na bila kificho uadui wake kwa nchi za eneo. Msemaji wa Jumuiya ya Kiislamu ya Colombia ameongeza kuwa, Israel sio tu kwamba, inamiliki silaha za kemikali bali inazo pia silaha za nyuklia ambazo ni tishio kubwa kwa usalama wa dunia hususan eneo la Mashariki ya Kati. Rashid Caravali amesema, jamii ya kimataifa inapaswa kuushinikiza utawala huo ghasibu ili uangamize silaha zake zote za atomiki na kwa muktadha huo eneo la Mashariki ya Kati litashuhudia amani na utulivu.

Al-Mualim: Mpango amani umshirikishe Assad

Al-Mualim: Mpango amani umshirikishe Assad



Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria amesema kuwa, serikali ya Damascus haitokubali mpango wowote wa amani wa kukabidhi madaraka kwa ajili ya nchi hiyo ambao hautomshirikisha Rais Bashar al Assad.

Matamshi ya Rais wa Tunisia yaighadhibisha Imarati


Matamshi ya Rais wa Tunisia yaighadhibisha Imarati


wwwbinhafidhi


Umoja wa Falme za Kiarabu, Imarati umemwita nyumbani balozi wake wa nchini Tunisia kulalamikia wito wa Rais wa nchi hiyo Moncef Marzouki kutaka Muhammad Morsi, rais wa Misri aliyeondolewa madarakani na jeshi na kuwekwa kizuizini hadi sasa, aachiliwe huru. Akihutubia mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa juzi Alkhamisi, Rais wa Tunisia aliwataka watawala wapya wa Misri wanaoungwa mkono na baadhi ya nchi za Kiarabu ikiwemo Imarati wamwachie huru Rais halali wa nchi hiyo Muhammad Morsi aliyeondolewa madarakani Julai 3 katika mapinduzi yaliyoongozwa na jeshi. Gazeti la Al- Khaleej linaloakisi misimamo ya serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu limekosoa hotuba ya Rais wa Tunisia kwa kuishambulia serikali ya mpito ya Misri na kusisitiza kuwa kinachotakiwa kufanywa ni kuiunga mkono serikali ya Cairo ambayo imekuja madarakani kwa matakwa ya wananchi. Baada ya jeshi kumuondoa madarakani Morsi, Umoja wa Falme za Kiarabu, Saudi Arabia na Kuwait ziliunga mkono mapinduzi hayo na kuahidi kuipatia kwa pamoja Misri msaada wa dola milioni 12 kusaidia uchumi wake uliozorota…/

Mashambulizi ya ash- Shabab katika kambi ya wakimbizi ya Daadab Kenya






wwwbinhafidhi.blogspot.comWimbi la mashambulio ya kundi la ash- Shabab la Somalia katika nchi jirani lingali linaendelea. Katika hatua yao ya hivi karibuni wanamgambo wa ash- Shabab wameshambulia kambi ya wakimbizi ya Daadab huko kaskazini mwa Kenya. Ripoti zinaeleza kuwa watu watatu wameuliwa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mashambulizi hayo. Imeelezwa kuwa wafanyakazi wa shirika moja la kimataifa la huduma za kibinadamu pia wamelengwa kwa mashambulizi hayo ya ash-Shabab.
Kambi ya wakimbizi ya Daadab iko katika mpaka wa Kenya na Somalia na ndio kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani. Maafisa usalama wa kieneo wameeleza kuwa wavamizi wa ash-Shabab walikuwa wamejizatiti kwa silaha za aina mbalimbali na mada za milipuko na waliingia kwa nguvu kambini hapo. Kambi hiyo inawahifadhi wakimbizi wengi wa Kisomali wasio na ulinzi waliokimbia ukame na mapigano ya ndani nchini kwao.
Jumamosi iliyopita pia watu wengi waliuliwa na wengine kujeruhiwa katika mashambulizi yaliyofanywa na kundi hilo hilo la ash-Shabab katika jengo la maduka la Westgate jijini Nairobi, Kenya.
Tangu mwaka jana wanamgambo wa kundi la ash-Shabab walianza kupoteza ngome zao muhimu nchini Somalia na kulazimika kurudi nyuma baada ya kupata kipigo kutoka kwa vikosi vya majeshi ya Umoja wa Afrika vilivyopelekwa nchini humo kusaidia serikali ya Mogadishu. 
Wakati huohuo kufukuzwa wanamgambo wa ash-Shabab katika bandari ya kistratijia ya Kismayu ambayo ilikuwa moja ya ngome zao kuu, kulikuwa na umuhimu mkubwa. Hii ni kwa sababu sehemu kubwa ya mahitaji ya silaha na chakula ya wanamgambo wa ash-Shabab ilikuwa ikidhaminiwa kupitia bandari hiyo.
Harakati za kundi hilo la ash Shabab zimezilazimisha nchi mbalimbali za Kiafrika kuchukua tahadhari kubwa za kiusalama. Huko Uganda vikosi vya usalama vimejiweka tayari kwa ajili ya kukabiliana na mashambulizi yoyote yanayoweza kufanywa na kundi hilo. Miongoni mwa hatua hizo ni kufungwa kamera kwenye maeneo ya umma, barabarani na katika baadhi ya majengo na vilevile kuimarishwa hatua za kiulinzi kwenye mipaka ya Uganda.
Uganda ni miongoni mwa nchi zilizochangia wanajeshi katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika huko Somalia. Kundi la ash-Shabab linapinga vikali uingiliaji wa vikosi vya majeshi ya kigeni huko Somalia na linataka vikosi hivyo viondoke katika ardhi ya nchi hiyo. Awali wanamgambo wa ash-Shabab walitishia kwamba watalipiza kisasi iwapo vikosi vya nchi za kigeni havitaondoka Somalia.
Mlipuko wa bomu uliotokea Kampala mji mkuu wa Uganda wakati watu walipokuwa wakitazama fainali za mpira wa miguu za Kombe la Dunia mwaka 2010 zilizofanyika Afrika Kusini na kuua  watu 76, ni mfano mmoja wa hatua za kulipiza kisasi za kundi la kigaidi la ash-Shabab huko Uganda. Wanamgambo wa ash-Shabab wamedai kuwa, wanajeshi wa Kenya wameondoka huko Somalia kutokana na hali mbaya ya usalama inayoikabili Kenya, madai ambayo yamekadhibishwa na viongozi wa Nairobi.  
Swali linaloulizwa kwa sasa ni kuwa, ni nani anayewafadhili na kuwadhaminia wanamgambo wa ash-Shabab silaha na mahitaji mengine muhimu?  Wakati huo huo weledi wa mambo wanasema kuwa ukosefu wa amani katika eneo la Pembe ya Afrika unayafaidisha madola ya Magharibi ambayo yatatumia fursa hiyo kwa ajili ya kuingilia masuala ya ndani ya nchi za eneo hilo.

Mlipuko waua watu 6 huko Tumbuktu Mali


Mlipuko waua watu 6 huko Tumbuktu Mali

Watu 6 wameuawa wakiwemo raia wawili na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia mlipuko uliotokea karibu na kambi ya jeshi katika mji wa kihistoria wa Timbuktu nchini Mali. Afisa wa serikali katika eneo hilo ameeleza kuwa, mlipuko huo wa kutegwa garini umesababisha pia nyumba kadhaa kuporomoka na kutokea hasara kubwa.
Serikali ya Mali imelaani shambulio hilo lililotokea ikiwa zimepita siku chache tu tangu waasi wa Tuareg wanaopigana ili kulitenga eneo la Kaskazini wasimamishe mazungumzo na serikali, wakiituhumu kwamba imeshindwa kuheshimu makubaliano ya amani yaliyofikiwa kati ya pande mbili. Mwezi Juni viongozi wa kundi la Tuareg walifikia makubaliano na serikali ya mpito ya Mali yaliyopelekea kurejea jeshi kwenye mji wa Kidal na kufanyika uchaguzi wa rais.

Serikali ya Kenya imesema nchi iko katika vita na wapiganaji wa Somalia, al Shabaab.


Wakenya wakiomboleza kwa kuwasha mishumaa nje ya Westgate

Imekanusha kuwa vitisho vya mashambulio vinavotolewa na kundi hilo vilipuuzwa.
Jumamosi usiku wafiwa na marafiki walioonesha majonzi waliwasha mishumaa nje ya Westgate kuwakumbuka waliokufa.Inajulikana kuwa watu 67 walikufa katika shambulio la Westgate, liloendelea kwa siku nne.
Magazeti ya Kenya yameandika ilani inayodaiwa kutolewa na idara ya usalama mwaka mmoja uliopita kuhusu watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa al-Shabaab mjini Nairobi ambao wakipanga mashambulio ya kujitolea mhanga, piya katika jengo la maduka la Westgate.
Magazeti ya Kenya yameuliza iwapo wakuu walishindwa kuchukua hatua baada ya onyo hilo na mengine yaliyofuata; pamoja na onyo moja kwamba kutafanywa mashambulio sambamba mijini Nairobi na Mombasa baina ya tarehe 13 hadi 20 Septemba.
Kamati ya bunge itayokutana Jumatatu imeonesha inataka kutazama swala hilo la ilani hizo zilizotolewa.
Afisa mmoja mwandamizi wa wizara ya mambo ya ndani alisema serikali inapata taarifa kama hizo kila siku.
Hatua zimechukuliwa kuepusha mashambulio mengi.
Alisema Kenya iko vitani, na kila siku kijana wa Kenya anashawishiwa na al-Shabaab kuuwa Wakenya.

boko haram la shambulia nigeria


Ramani ya Nigeria

wwwbinhafidhi.blogspot.comJeshi la Nigeria linasema watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Kiislamu wa kundi la Boko Haram wameshambulia wanafunzi waliolala katika chuo cha kilimo katika jimbo la Yobe, kaskazini mwa nchi.
Inaarifiwa kuwa wapiganaji waliwafyatulia risasi wanafunzi wa chuo hicho katika eneo la mashambani la Gujba.
Inaarifiwa piya kuwa walichoma moto madarasa .
Duru za hospitali kaskazini-magharibi mwa Nigeria zinasema watu kama 26 wameuwawa katika shambulio hilo.